Mindyou
JF-Expert Member
- Sep 2, 2024
- 1,869
- 4,877
CHADEMA imetoa mapendekezo matatu kwa serikali kufuatia uamuzi wa Rais wa Marekani,Donald Trump kusitisha misaada kwa sekta ya afya.
Mwenyekiti wa Kamati ya Afya na Maendeleo ya Jamii ya Bunge la Wananchi CHADEMA, Ashura Masoud, lazima hatua zifuatazo zichukuliwe kukabili mabadiliko hayo.
1. Chama hicho kimependekeza serikali kuandaa mkakati wa dharura wa kisera na kibajeti wa kuhakikisha inakuwa na fedha za kutosha kwenye Mfuko wa Kudhibiti UKIMWI na Mfuko wa Udhamini wa UKIMWI kwa kubana matumizi na kutenga vyanzo maalum na vya lazima katika bajeti ya taifa,ili kupunguza makali ya uhaba wa fedha za ARVs na UKIMWI.
2. Bunge linaloendelea sasa kujadili ajenda ya dharura,serikali iwasilishe taarifa ya tathimini na mkakati wa kina wa namna ya kukabiliana na upungufu wa fedha katika sekta ya afya na nyingine za maendeleo,kisha litokea na azimio.
3. Rais Samia Suluhu Hassan na wakuu wenzake wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Umoja wa Afrika (AU) wafanye mkutano kwa ajili ya kutafuta ufumbuzi mpana na wa kina zaidi kupata vyanzo mbadala vya fedha na kuziba pengo la kibajeti linalosababishwa na Marekani kusitisha misaada ya maendeleo.
Aidha,amesema: " Tathimini iliyofanywa na Kamati ya Afya ya Bunge la Wananchi imebaini kusitishwa kwa misaada hii kutaathiri huduma ya ARVs pamoja na mapambano dhidi ya VVU na UKIMWI KWA asilimia 50."
Source: Nipashe