Chadrack Issaka Boka Mayday Mayday Mayday!

Chadrack Issaka Boka Mayday Mayday Mayday!

MwananchiOG

JF-Expert Member
Joined
Apr 4, 2023
Posts
1,970
Reaction score
4,037
GYB1PdvWsAAAW7z.jpeg

Mayday ni neno la utaratibu wa dharura linalotumiwa kimataifa kama ishara ya dharura katika mawasiliano ya redio. Kwa wale wanaofahamu mambo ya jeshini nadhani watakuwa wanafahamu, hususan anga.

Hutumika kuashiria hali ya hatari inayohatarisha maisha ya wasafiri wa anga, lakini katika baadhi ya nchi mashirika ya ndani kama vile wazima moto , vikosi vya polisi , na mashirika ya uchukuzi pia hutumia neno hilo kuashiria hali ya hatari imeibuka na msaada wa haraka sana unahitajika. Makubaliano ya matumizi ya neno hilo unahitaji kurudiwa mara tatu mfululizo wakati wa tangazo la dharura la awali ("Mayday mayday mayday") ili kurahisisha mawasiliano ambayo yanaweza kukatizwa na muingiliano wa mawimbi.

Chadrack Issaka Boka, Mchezaji mwenye mbio mithili ya duma, mpaka kufikia baadhi ya mashabiki kukiri kwamba huenda alipaswa kushiriki olympiki mbio za mita fupi, wengine wakifika mbali kushukuru kuwa mchezaji mpira maana angekuwa kibaka hakika kwa hizo mbio asingekamatika, wengine wakisema labda boka anafukuzwa na mbwa asiyeonekana huku wengine tukidhani anakimbiza mpira!

Naam, chini ya Miguel Gamondi, Chadrack boka anayevaa jezi namba 23 amepewa jukumu moja tu, mikimbio + kumwaga maji, Japo wengine wakisema hatekelezi vyema majukumu yake kwani badala ya kumwaga maji, Yeye ana mimina upupu!

Mayday! mayday! mayday! Ni kelele za kuomba msaada kutoka kwa wapinzani, pale Chadrack boka anapogusa mpira, Maana yake ni kwamba, hali ya HATARI imetokea! Msaada wa haraka sana unahitajika kabla balaa halijatokea! Maana yake ni kwamba sekunde 8 ni nyingi kabla huyu kiumbe mwenye mbio mithili ya mbwa mwizi hajamwaga upupu na kuzua balaa! Picha linaanza kwanza bukta imekunjwa kama wale wanariadha wa miaka ya 80! 😀 Akishika mpira timu pinzani wote inabidi wakusanyane haraka kwa dharura kudhibiti maji!

Naam huyu ndiye Chadrack issaka boka mapafu ya Ngiri

GYBhNNGXMAA3WKu.jpeg
 
Hata defensive amebadilika mno kama jana ulifuatilia mchezo alikuwa anapanda sana
 
Jamaa kwasasa ananikosha sana anatimiza majukumu yake kwa ufasaha kabisa anakaba na kushambulia kwa weledi mkubwa jana kanikosha sana..
 
Watu msichojua huyu jamaa umri umesogea sana na anakuwa na pancha sana. Mtakuja kuniambia hapa huyu sio 23
 
Back
Top Bottom