Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
CHAGGA DAY
TUIKUMBUKE SIKU HII KWA KUREJEA KATIKA MAISHA YA RAJABU IBRAHIM KIRAMA NA BABA YAKE MURO MBOYO KATIKA MIAKA YA 1800
Chagga Day ni siku iliyokuwa ikiadhimishwa kila mwaka ifikapo tarehe 10 Novemba na kwa hakika ilikuwa sikukuu kubwa sana.
Sherehe zikifanyika Chagga Council Kiborloni.
Wachagga toka zama hizo walijihisi na kujiona ni taifa na ardhi yao yote ni nchi kamili.
Nchi yenye mipaka yake ya kueleweka.
Wenye lugha moja lau kama makabila yao ni mengi na yakiishi sehemu mbalimbali chini ya mlima.
Ulikuwa wakati wa watawala (Mangi) mfano wa Mangi Ndeseruo Mamkinga wa Machame na wale waliomfuata katika kiti hicho Shangali Ndeseruo na Abdiel Shangali.
Pamoja na hawa watawala wenye sifa alikuwapo Muro Mboyo, Jemadari wa majeshi ya Mangi Ndeseruo Mamkinga, Muro Mboyo na mwanae Rajabu Ibrahim Kirama.
Hii ilikuwa kutokea miaka ya katikati ya 1800 kuingia 1900.
Kilimanjaro uliwaongezea Wachagga mapenzi kwa nchi yao kwa ajili ya ule uzuri wake.
Mlima umesimama ukiinamia ardhi yote; hasa unapokuwa haujafunikwa na mawingu kwani kuna siku Wachagga huamka na wasiuone mlima.
Wachagga wanaamini bila Mlima Kilimanjaro hakuna Wachagga.
Na hakika kabisa unaweza mtu ukafikiria na kusema kuwa, Mlima Kilimanjaro ni nembo ya matumaini makubwa wa ustawi wa Wachagga.
Mlima pia ni sawa na alama inayomuonesha rafiki au adui, walipo Wachagga.
Ikiwa una haja nao na unawatafuta iwe kwa kheri ama kwa shari.
Kwa anayekuja, kokote anapotokea iwe kutoka pwani ya mbali za ardhi ya Wachagga; au nyuma ya mlima, kutokea Kenya, Mlima Kilimanjaro utaonekana umesimama hausogei pale ulipo.
Na kila unapoukaribia ndipo unapozidi kujidhihirisha ukubwa na uzuri wake.
Umuhimu wa Muro Mboyo ilikuwa kuona kuwa yeye bila shaka ndiye alikuwa na mengi ya kuhadithia katika historia ya Machame ni kuwa aliishi akashuhudia kwa macho yake mwenyewe taratibu nguvu za utawala wa ukoo wa Mangi Shangali nchini kwake Machame ukipotea na utawala mpya wa wakoloni Wajerumani ukiingia Uchaggani pote.
Bila shaka mabadiliko haya yalimsababishia Muro Mboyo simanzi kwa kukumbuka historia ya nguvu ya ukoo wake, wa majemadari wa vita, ukipotea na kuchukuliwa na wageni kutoka mbali kwenye nchi ambayo hakupata kuijua wala kuisikia.
Wageni hawa wakaja na utawala mpya na silaha mpya za vita zenye nguvu kubwa ya kuua na kuangamiza kutoka mbali.
Wageni hawa kutoka Ulaya pia wakawaeleza kuwa Mungu wa Wachagga si Mungu ila Mungu wa kweli ni Yesu Kristo wa Nazareth.
Si yule Mungu wao aishie Mlima Kilimanjaro kwenye vilele vya Kibo na Mawenzi.
Muro Mboyo alimweleza mwanaye Kirama historia hii ya Wachagga kama njia moja ya kufuta aibu iliyomgubika yeye binafsi na kwa hakika Wachagga wote ya kujikuta wao ni taifa lililo chini ya utawala wa taifa jingine la watu weupe.
Muro Mboyo hakuwa tena na majeshi ya kuongoza yakimfuata nyuma vitani kulinda utawala wa Shangali.
Muro Mboyo kuikumbuka historia ya wazee na kumuhadithia mwanae Rajabu Kirama ilikuwa moja ya njia ya kupata faraja na kurejesha heshima yake na ya watu wake kama vile kusema kuwa na sisi tulikuwa taifa kama wao Wajerumani.
Kwa miaka mingi Chagga Day ilibaki kuwa siku ya kukumbuka Taifa la Wachagga na sikukuu hii ilimalizikia na Paramount Chief Thomas Marealle baada ya Tanganyika kuwa nchi huru.
Picha: Mangi Shangali Ndeseruo, Rajabu Ibrahim Kirama, Chief Abdiel Shangali na Mangi Mkuu Thomas Marealle.