Bado tuna safari ndefu sana kuelekea kuwa na kizazi kitakachokuwa kinapiga kura kutokana na sifa na utendaji wa wagombea (based on merits) na sio kanga, T-shirt na pilau. Sidhani kama wananchi walio wengi (70% kama alivyosema Mh. Rais JK) wanajua maana ya Uchaguzi.
Ndio maana CCM badala ya kukaa na kutafakari mbinu mpya za kuleta maisha bora kwa kila mtanzania (mbinu zilizopo zimefeli kabisa) wanaagiza Toyota Landcruiser 150 kwa ajiri ya kubebea wapambe, kanga, kofia, TOT na T-shirt!!
Laiti kama hawa 70% wangejua maana ya kupiga kura na impact yake, basi 2010 tungeshuhudia mtikisiko wa kisiasa Tanzania!!