Uchaguzi 2020 Chagua Tundu Lissu kwa Bara, Chagua Maalim Seif kwa Zanzibar

Uchaguzi 2020 Chagua Tundu Lissu kwa Bara, Chagua Maalim Seif kwa Zanzibar

MAHANJU

JF-Expert Member
Joined
Aug 26, 2014
Posts
5,252
Reaction score
8,003
Hakuna sababu ya kuendelea kulia lia na ugumu wa maisha. Tuchague Tundu Lissu kwa kishindo upande wa Bara na Maalim Seif upande wa Visiwani. Tunayo hatima ya Tanzania mpya inayojali haki, uhuru na maendeleo ya watu badala ya Tanzania ya maumivu zaidi isiyojali haki wala maendeleo watu aliyosema mwalimu Nyerere.

Tusitoe mwanya kwa CCM ambayo haieleweki kua awamu ijayo wanaweza kujiongezea muda wa kukaa madarakani maana walishaamua kujiandaa na hilo. Tuwakatae hawa hawana nia njema na maisha ya watanzania hawa.
Tuchague viongozi watakaosimama na haki kwa watanzania wote bila kujali uwezo wao.

CCM tangu tupate uhuru wameichelewesha maendeleo nchi hii, hali tuliyonayo siyo mahali ambako tulitakiwa kuwepo. Wamekua wakigawana keki ya nchi hii ndiyo maana mpaka sasa hazieleweki ziliko 1.5t.
 
Bahati mbaya mwaka huu upinzani mmetuletea mawakala tu. Bara tukiwa na wakala wa beberu, visiwani tuna wakala wa mwarabu.

Thamini na tambua uhuru wa nchi, kura kwa JPM na Mwinyi
Screenshot_20201024-110904_1.jpg
 
ASUBIRI TUUU KUGARAGAZWA YEYE NA WAGOMBEA UBUNGE WENZAKE. WATANZANIA HATUTAKI WACHEZEA RASILIMALI ZETU. AKIPATA ATA KULA 1000, ATAKUWA AMEJITAIDI
 
Watanzania wamechoka kutawaliwa na mkoloni na kaburu mweusi. Ni lazima tutafute mwanzo mpya kwa mustakabali wa Taifa letu. Chagua Tundu Lissu na Maalim Seif kwa ajili ya kesho nzuri ya maisha yako na familia yako.
 
Wakoloni weusi ambao ndio Hatari kabisa
 
Kura zote kwa Lissu na Maalim Seif! Matatizo yote tuliyo nayo ni matokeo ya kuongozwa na chama kisichokuwa na dira wala mawazo mapya, leo kinashika hili, kesho wanaacha kisha wanarukia kingine!
Chama kinajitapa kuwa kimeba ngao ya kutetea wakulima na wafanyakazi , lakini miaka zaidi ya 50 toka tupate uhuru, wakulima na wafanyakazi wapo hoi kiuchumi wakati viongozi na wanachama wa CCM wanaogelea kwenye matumizi ya anasa, wanatembelea mashangingi wakati wameshindwa kutoa milioni 50 hata kwa kijiji kimoja tu!
Hapana ni lazima tuikatae CCM, Kesho twende sote tukapige kura nyingi kwa Lissu na Maalim Seif ndio wakombozi wa Tanzania ilipokwama!
 
Tree TT
 
Back
Top Bottom