Chagua Watatu Bora Kuwahi Kuvaa Jezi Namba 10

Greatest Of All Time

JF-Expert Member
Joined
Jan 1, 2017
Posts
23,620
Reaction score
52,790
Umepewa nafasi ya kuchagua wachezaji watatu bora kuwahi kuvaa jezi namba 10 kwa levo ya klabu, chaguo lako ni lipi?

Mimi naenda hivi...
1.Messi
2.Rui Costa
3.Modric
 

Attachments

  • IMG_20191010_210045.jpeg
    103.5 KB · Views: 2
1.Jari Litmanen hasa yule wa Ajax
Aliibeba Ajax ya Louis Van Gaal kwenye mabega yake.

2.Roman Riquelme
Dunia ya soka haikuwahi kumpa credit zake.
Kontroo yake maridadi mno. Timing na movement zake ni level za juu sana.

3.Wayne Rooney
Wengi hupenda kumuita Pele mweupe, anakuofa vitu vingi, nguvu, akili, jihadi. Sema tu kwakuwa alicheza katika zama za Messi na Ronaldo. Wazza ni one of the most underrated player of all time.
 
Dah! Nimemkumbuka Huyo Mwamba wa Argentina akiitwa Roman Riquelme.
 
Dah! Nimemkumbuka Huyo Mwamba wa Argentina akiitwa Roman Riquelme.
Aliuwasha moto akiwa na Vilareal C.F au nyambizi ya manjano.

Alikuwa ni sehemu ya kikosi cha Villareal kilichofika nusu fainali ya UCL msimu wa 2005/2006 huku wakitolewa na Arsenal.

Baadhi ya wanandinga wengine ni pamoja na kiungo fundi Santi Carzola, kiungo mkabaji bora kwa msimu huo Marco Senna, mshambuliaji wa Uruguay Diego Forlan naye alikuwepo kikosi, bila kumsahau Nahodha Pablo Sorin kutoka Argentina na nywele zake style ya Forlan.

Hilo kosi lipo chini ya jemedari Manuel Pellegrin "El Enginielo" The Engineer.
 
Litmanen
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…