Nimekuwa kimya nikisikiliza kila wadau wanapotoa na kujenga hoja zao za ama serikali mbili au serikali tatu; binafsi nakosa mantiki ya nini hasa makundi haya yanachopigania; ila kama wote tunalenga kuuimarisha Muungano na kuijenga Tanzania iliyo bora zaidi na yenye mshikamano, nadhani sote tuko upande mmoja na tunafikiria jambo ambalo ni zuri kupindukia.
Kumbe kama ni hivyo kwa mwenye kuielewa maantiki hiyo hangelisita kupigia chapio kuwe na Serikali moja yenye kutunza maslahi ya pande zilizounda Muungano wa serikali hii.
Lakini mimi kwa uelewa wangu ninaangalia mambo mawili muhimu katika matukio ya nchi yetu hii:
I. Mwaka 1962 vyama vingi vya siasa vilifutwa kwa maslahi yaliyokuwepo enzi hizo. Na Marehemu Baba wa Taifa Mwl JK Nyerere aliekuwa Kiongozi wa Nchi yetu alikubaliana na uamuzi wa kuwa na chama kimoja tu cha siasa na kulisimamia hilo kwa umakini na ukamilifu wote. Mwaka 1989 wakati wananchi na hasa wanachama wa CCM wakihojiwa kuanzishwe vyama vingi vya siasa ama hapana, iliezwa matokeo yalikuwa asilimia 80 walisema hapana na waliokubali kuwe na vyama vingi vya siasa wakawa 20% tu. Lakini uhalisia wa kisiasa uliokuwepo wakati huo mwaka 1989 ulikuwa tofauti na matokeo ya kura. Mwalimu aliwaeleza Watanzania akiwafumbua macho kuwa pamoja na wingi wa Wana CCM waliokataa kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi vya siasa, aliwaambia "hilo kwa sasa HALIEPUKIKI, kwani sababu zilizoifanya nchi iwe na mfumo wa chama kimoja za mwaka 1962 hazipo tena na hazibebi uzito wowote kwa enzi za wakati huo". Matokeo yake mwaka 1992 mfumo wa vyama vingi ulianza.
II. Sikumbuki mwaka ila nakumbuka kipindi Fulani kulifumuka kundi ndani ya Bunge lililojiita G8. Hawa G8 walikuwa watetezi wa kuanzishwa upya serikali ya Tanganyika. Kundi hili lilikemewa sana na Baba wa Taifa Mwl JK Nyerere akidai kuwa walikuwa hawana uhahali wowote wa kudai kitu kama kile na kwamba walikiuka kuilinda katiba ya nchi kama walivyokuwa wameapishwa. Nami nasema Mwl alikuwa sahihi 100% kwa kuwakemea hao, kwani hao walifumuka tu pasipo utaratibu maalumu uliondaliwa wa kwenda na hoja ya jambo nyeti kama hilo.
Leo hii yeyote anayekataa kudai muundo bora kabisa wa serikali ya Tanzania baada ya Rais kuunda chombo cha kuandaa katiba mpya ya nchi yetu ambacho ndio utaratibu Mwalimu alikuwa anaueleza kuwa haukuwepo, atakuwa haitendei haki Tanzania. Tume ya mabadiliko ya Katiba imekuja na mapendekezo bora kabisa yaliyotoka kwa wananchi na yaliyofanyiwa utafiti wa kina ya muundo ulio bora kabisa wa serikali yetu. Mimi binafsi ninaamini kuwa Mwl angekuwepo leo kwa utaratibu huu uliofanyika hangesita katika kumuunga mkono Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Mhe Jaji Warioba kwa kutofautiana na wajumbe wengi wa Chama cha Mapinduzi; Kama ilivyokuwa kwa vyama vingi na chama kimoja.
Bado naamin Mwalimu aliyekuwa mmojawapo wa waasisi wa Muungano baina ya Tanganyika na Zanzibar pamoja na Mzee wetu Marehemu Sheikh Amri Abeid Amani Karume mwaka 1964; Kama alivyowafumbua macho Watanzania mwaka 1989 wakati ule ili tuwe na vyama vingi vya siasa ama la, leo pia angewafumbua macho tena Watanzania mara baada ya rasimu ya pili kukabidhiwa na angewaambia "Wenzetu wanaoenda bunge la Katiba wachague moja kati ya haya, Serikali moja ama Serikali tatu" hiyo ni kulingana na UZITO wa hoja za Wananchi walizozitoa mbele ya Tume.
Mimi nimelonga ya kwangu, lakini chaguo la serikali mbili MBELE kuna giza NENE.
Kabengwe@jamiiforums.com