Chaguzi feki zitaiua hata CCM yenyewe

Chaguzi feki zitaiua hata CCM yenyewe

Missile of the Nation

JF-Expert Member
Joined
May 24, 2018
Posts
15,101
Reaction score
56,054
Kuna wana CCM wanafurahia uhuni wanaofanyiwa wapinzani kwenye chaguzi. Kwao inawapa sense ya ufahari ya kujiona wana power fulani hivi inayowawezesha kuiruhusu haki kwa kupenda au kuiminya haki kwa kupenda.

Hata hivyo huu ni mtazamo finyu. Ikifikia hatua ile core ya CCM ikaamini kuwa haihitaji kura za wananchi kukaa madarakani basi hiyo dhana haitaishia hapo, itawafanya waamini kuwa hawahitaji wanachama wa chini wa CCM ili waweze kukaa madarakani. Wao vyombo vya kuvipa attention itakuwa ni polisi, usalama wa Taifa, na pengine jeshi. Kwa hiyo wana CCM wanaodhani kuwavuruga wapinzani kwa kuiba kura kunawanufaisha basi nao wanajiumiza wenyewe.

Pia ili thamani ya wanaCCM hasa wa ngazi za chini ionekane, lazima uwepo upinzani ambao umechangamka. Hii itapelekea mchango wao ndani ya CCM uthaminiwe. Sasa ukiua upinzani, watakaonufaika na hali hiyo japo kwa muda mfupi ni viongozi wa juu wa chama. Ndiyo maana ni muhimu kwa wana CCM kukataa njia haramu zidizofair za kukwamisha upinzani kukua nchini.
 
Unanikumbusha diwani feki na mwenekiti wa mtaa feki utapata jamii feki.

UchaguzI feki=Jamii feki Jamii feki = uchaguzi feki
 
Back
Top Bottom