Chaguzi Kidato cha Tano na Vyuo vya Kati: Uraiani hakusomeki na soko la Ajira nalo halisomeki

Chaguzi Kidato cha Tano na Vyuo vya Kati: Uraiani hakusomeki na soko la Ajira nalo halisomeki

Joined
Apr 16, 2021
Posts
83
Reaction score
118
Kufuatia Machaguzi ya kwenda kujiunga na elimu ya kidato cha 5 na vyuo vya Kati. Nimeona wizara (TAMISEMI) imewapangia wanafunzi wengi sana kwenda kusoma vyuo vya kati.

Kwa kozi zingine ambazo ukiziona unaanza kumuonea dogo huruma. Mfano: Public Administration, Tour Guide, ualimu, Business Administration, Secretarial Course, Investment and Risk Assessment.

Swali langu ni je, hawa wanafunzi waliopangiwa wana uelewa mpana na hicho wanachoenda kusoma? Na je, serikali wana nia gani au wana mfumo na mpango upi wa kuwasaidia hawa wadogo zetu pindi watakapohitimu hizo kozi zao?

Kutokana na changamoto za ajira ningependekeza serikali iwachagulie vyuo vya ufundi zaidi kuliko hizo course baadhi walizopelekwa kwani huku uraiani hakusomeki na soko la Ajira nalo halisomeki.
 
Mkuu upo sahihi sana, serikali ya Tanzania bado haijawa serious na wadogo zetu. Kama unamchagulia mwanafunzi course ambayo kupata ajira ni mtihani sana lakini pia yeye kujiajiri ni shida hiyo course itamsaidia nini?
 
Back
Top Bottom