Chaguzi tunazofanya

Chaguzi tunazofanya

Shayu

Platinum Member
Joined
May 24, 2011
Posts
608
Reaction score
1,655
Mwenye busara hutumia hekima kwanza kabla ya nguvu. Faida ya kutumia hekima kabla ya nguvu uwapa ufahamu wale wanaotakiwa nguvu itumike kwao ili wajielewe.

Na kujielewa ni jambo ambalo taifa lolote linahitaji kwa watu wake. Kuongoza ni kufanya watu wako wajielewe huwezi kuongoza watu wasiojielewa hivyo inahitaji vision kuongoza watu.

Watu wanaojielewa wana perfom vizuri zaidi katika majukumu yao na ya taifa lao kuliko wale wasiojielewa.

Kwahiyo upumbavu ni jambo ambalo tunapaswa kupambana nalo. Upumbavu unalala kwenye mwenendo ndio unaonyesha huyu mpumbavu au sio mpumbavu. Hata mwenye elimu ya darasani anaweza kuwa mpumbavu kutokana na choices anazofanya katika maisha yake na mwelekeo wa fikra na matendo yake.

Binadamu ana asili mbili ndani yake, Wema na uovu. Inategemea ni ipi inasaidiwa kukua ndani yake. Mawazo yetu na matendo husaidia kati ya hizo asili mbili kukua. Na Malezi ambapo mzazi hu suppress bad nature na kusaidia kukua good nature ya mtoto. Au kuruhusu bad nature kukua iwe kwa kutokuwa makini au kuipalilia makusudi.

Malezi ya awali ni muhimu katika kujenga raia bora na good nature ya mtu.

Jinsi unavyofikiri na kutenda kunaelezea kila kitu juu yako. A lack of discernment to make a choice between right and wrong ndiko kunakomfanya mtu mpumbavu. Na madhara ya upumbavu ni maangamizi iwe kwa mtu mmoja mmoja au kama jumuia na Taifa.


Kwahiyo jambo la msingi hapa kama taifa ni kupambana na upumbavu ili tuwe na raia wanaotenda katika usahihi ( right actions) kwasababu dira yetu kama taifa inategemea hilo.

Mataifa yanapoingia kwenye vita na machafuko ni sababu ya matendo yao. Sababu ya choices zao na mwelekeo walioamua kuchukua kama taifa. Wrong choices always bring people kwenye disaster. And right actions kwenye utulivu na amani.

Na mithali hii ni kweli tutavuna tulichopanda. Mwisho wetu unategemea mwelekeo wa matendo yetu.

Na kumbuka kila siku tunatembea tukikikaribia kifo, tunakuwa watoto, vijana, wazee kwenye safari hii ya kukikaribia kifo kisha tunafutika kwenye uso wa dunia. Matendo yetu hubaki nyuma yetu mabaya au mazuri.

Hakuna mtu kati yangu mimi na wewe atakayebaki duniani milele. Kitu cha kufariji ni kwamba we leave our offspring behind . Only copy of ourselves. That is only thing we can hope. It is our only hope. Ili kizazi cha binadamu kisipotee. Kwasababu dunia bila binadamu ni dunia ya namna gani?

Lakini ukweli ni kwamba katika matendo yetu yote; mabaya kwa mazuri hayadumu sana zaidi ya yale yaliyotendwa kwa upendo. Hayo hubaki mioyoni mwa watu daima. Kwahiyo hatuna budi kutenda kwa upendo.

Chaguzi tunazofanya ndizo hutengeneza mwisho wetu.
 
Back
Top Bottom