Chaguzi za serikali za mitaa ni udanganyifu na uwizi

Chaguzi za serikali za mitaa ni udanganyifu na uwizi

BONTABOY

JF-Expert Member
Joined
Nov 20, 2015
Posts
234
Reaction score
238
Naanza kwa samahani siyo mwandishi mzuri. Cha msingi, ujumbe ufike moja kwa moja kwenye hoja.

Nilitaka kushiriki chaguzi za mitaa zilizopita, nikanyimwa kupiga kura kisa sina kadi ya chama. Hivi kila Mtanzania ana chama, hili suala ni lazima. Mbona chaguzi za mbunge, Rais na diwani hazina utaratibu huo? Na inawezekanaje watu kuongozwa na kiongozi ambaye hawakumchagua na wala hana sifa, ila anajulikana kwenye chama tu?

Hili ni jambo la ajabu sana linafanyika kwenye chaguzi za serikali za mitaa. Tunaomba hili liangaliwe kwa makini, lina ukakasi.
 
Inashangaza sana kila mgombea wa upinzani eti alikosea kujaza fomu kwa kutojua kusoma na kuandika. Wengine walienguliwa kwa kuwa tu walitumia anwani za posta ambazo si za vyama vyao mfano masanduku ya halmashauri. Uchaguzi wa 2019 kuna watu wanatakiwa wakaombe toba lasivyo hasira ya Mungu iko juu yao.
 
Mbona mmoja alishaungama kwa mtumishi wa Mungu kwa madhambi yake ya kudhulumu watu

Mungu nae hana hiana anashuhulika nao,amewajaza hofu,maradhi,kibri,masononeko,sukari. Pia figo,maini na mabandama vyote vinawapwita
 
Back
Top Bottom