Green tea hutengenezwa kutokana na mti wa kawaida unaotumiwa kutengeneza majani kama yale tunayotumia kila siku. Tofauti yake na majani ya kawaida ya chai ipo katika utayarishaji au utengenezaji wenyewe kiwandani. Zipo aina nyingi za chai mfano ni hii green tea, black tea(ambazo ni zile za kawaida kama chai bora, greenlable, tausi nk hapa kwetu), pia kuna white tea, yellow tea nk. Hivyo kimsingi chai hizo zote hutokana na mti mmoja tu uitwao kwa jina la kisayansi Camellia sinensis. Tofauti huja wakati wa uchakataji ambapo kila aina ya chai ina viwango tofauti vya uchakataji.
Hatua ya uchakataji iitwayo Oxidation ambapo chai hupashwa joto kali ndiyo huifanya chai kuwa na rangi aidha kijani(green), yellow au white. Na kwa green tea, yenyewe mchakato huu hufanywa kidogo sana na ndiyo sababu utakuta chai hii haipotezi ile rangi yake ya asili yaani kijani, wakati chai ya kawaida(black tea) yenyewe hupashwa joto kali(higher oxidation) mpaka kubadilika rangi yake ya asili na kuwa black(nyeusi).
Inasemekana chai ya kijani ina faida nyingi kiafya, na hutumiwa sana na Wachina, Wajapani na watu wengi kutoka bara la Asia. Green tea kwa hapa Tanzania inapatikana maduka mengi na super markets ila watu wengi hawajui, hudhani green tea ni kitu tofauti sana na majani yale ya kawaida. Paketi zake zimeandikwa Green Tea na karibu kampuni zote zinazotengeneza majani ya chai zina brandi zao za green tea. Unapotia green tea kwenye maji ya moto hutoa rangi ya kijani kama mchaichai lakini yenyewe siyo mchaichai bali ni majani ya chai hayahaya ya kawaida yanayolimwa Milimani Mufindi na Njombe.