zamuhalelu
Senior Member
- Oct 5, 2017
- 140
- 138
Kiongozi nilikuwa napiga sana mchai chai nikijua ndo hyo daaaah mwisho mkojo nao unasadifu rangi ya mchai chai kumbe sioo kiongozi doooh...Kuna majani yanaitwa green tea
Kwa hvyo mkuu nijilie huu mchai chai kwa utulivu kabisaaa?Ukiacha brand ya majani kuna green tea
Nahisi ndio mchaichai, huwa wanatumia sana kwa matibabu mengi na kupunfuza uzito
MmmhuGreen tea hutengenezwa kutokana na mti wa kawaida unaotumiwa kutengeneza majani kama yale tunayotumia kila siku. Tofauti yake na majani ya kawaida ya chai ipo katika utayarishaji au utengenezaji wenyewe kiwandani. Zipo aina nyingi za chai mfano ni hii green tea, black tea(ambazo ni zile za kawaida kama chai bora, greenlable, tausi nk hapa kwetu), pia kuna white tea, yellow tea nk. Hivyo kimsingi chai hizo zote hutokana na mti mmoja tu uitwao kwa jina la kisayansi Camellia sinensis. Tofauti huja wakati wa uchakataji ambapo kila aina ya chai ina viwango tofauti vya uchakataji.
Hatua ya uchakataji iitwayo Oxidation ambapo chai hupashwa joto kali ndiyo huifanya chai kuwa na rangi aidha kijani(green), yellow au white. Na kwa green tea, yenyewe mchakato huu hufanywa kidogo sana na ndiyo sababu utakuta chai hii haipotezi ile rangi yake ya asili yaani kijani, wakati chai ya kawaida(black tea) yenyewe hupashwa joto kali(higher oxidation) mpaka kubadilika rangi yake ya asili na kuwa black(nyeusi).
Inasemekana chai ya kijani ina faida nyingi kiafya, na hutumiwa sana na Wachina, Wajapani na watu wengi kutoka bara la Asia. Green tea kwa hapa Tanzania inapatikana maduka mengi na super markets ila watu wengi hawajui, hudhani green tea ni kitu tofauti sana na majani yale ya kawaida. Paketi zake zimeandikwa Green Tea na karibu kampuni zote zinazotengeneza majani ya chai zina brandi zao za green tea. Unapotia green tea kwenye maji ya moto hutoa rangi ya kijani kama mchaichai lakini yenyewe siyo mchaichai bali ni majani ya chai hayahaya ya kawaida yanayolimwa Milimani Mufindi na Njombe.
Habari wana jf naomba kujuzwa
jee hivi chai ya kijani(green tea) ndiyo ule mchai chai unaopatikana sehemu nyingi ambao ukiuchemshia na maji chai inabadilika rangi au chai ya kijani ni ipi. ??
Green tea ni chai ya kijani kimsingi hata mchaichai ukiwa wakijani ukachemsha kama chai na ukatoa kijani ni chai ya kijani au "GREEN TEA" ORODHA YA MAJANI AMBAYO HUWEZA KUTUMIKA KAMA GREEN TEA -:Kiongozi nilikuwa napiga sana mchai chai nikijua ndo hyo daaaah mwisho mkojo nao unasadifu rangi ya mchai chai kumbe sioo kiongozi doooh...
Hii grean tea naipata maduka gani?
Achana na green tea zenye Caffein, endeleza Mchaichai ni tiba fresh sana ikiwa inaondoa tatzo la kusahausahau.Kiongozi nilikuwa napiga sana mchai chai nikijua ndo hyo daaaah mwisho mkojo nao unasadifu rangi ya mchai chai kumbe sioo kiongozi doooh...
Hii grean tea naipata maduka gani?
Mmmhu
ORODHA YA MAJANI AMBAYO HUWEZA KUTUMIKA KAMA GREEN TEA -:
mint green leaves ,lemon green leaves, rosemery green leaves hutumika kutengeza green tea isiyo na caffeinHuweza kutumika kama Green Tea, lakini siyo green tea.
Mkuu peter Agostino yupo sahihi.
Hizo ulizozitaja zinatumika kama chai kwa majina yake ,mfano mint tea ni chai ya mnanaa kama sikosei.