Chaka la simba halilali nguruwe

Tatizo siyo uvivu wa kusoma bali ni kuelewa mada wanazosoma. Ukiandika mambo ya kidaku udaku hata ukaweka page mbili watasoma zote! Kuna mwandishi mmoja huwa anaweka page hadi kumi ndefu sana za kiudaku hapa na huwa zinasomwa zote!
JF ya Leo siyo ya 2007-10
 
Watanzania Wengi Niwa Hovyo Sana Pamoja Na Mleta Mada Mwenyewe.

Hivi Nikuulize Wakati Mnapa Samia Umakamu Wa Rais Hamkujua Kuwa Kuna Uwezekano Wa Mkuu Wake Kutokuwepo Au Kushindwa Kuwa Na Uwezo Wa Kuendelea Kuongoza.CCM Siku Zote Huwa Siwaeleewi .Huyu Mama Nyie Ndiyo Mliompa Umakamu Wa Rais .Ina Maana Hamkuona Kuwa Hana Sifa Zakuongoza .Au Ndiyo ile Staili Yenu Yakutaka Mtawala Awe Na Nguvu Nyingi Ndiyo Sbb Mkateuwa Ambaye Atampa Nafasi Yakuonekana.
 

Mkandara,
Umezungumzia kwanini Mama Samia anatupa Ganda la Ndizi...ukimaanisha anawaondoa wasaidizi wa walioteuliwa na awamu iliyopita.
Swali ni je, Ganda la ndizi likiwa na makovu, uchafu pamoja na wadudu bado linakuwa na maana ya kutibu afya?
Ganda la ndizi haliwezi kuwa na wadudu bali wadudu hufuata tunda la ndizi. Ganda ni kinga ya tunda hivyo ganda likiwa na makovu bila shaka hata ndizi ina wadudu haifai. Leo ni miaka miwili tu, Mama kafanya teuzi ngapi vile?
 

Tatizo kubwa lililopo ni kuwa Mama alipo hayaoni mapungufu yake. Alipo anaamini yeye ni bora zaidi kuliko watangulizi wake na bora zaidi kuliko wote duniani.

Ninakazia:

"Haiwezekani kabisa Chaka la Simba (lion den) tunawaona hata nguruwe wakilala, hapo pana tatizo la msingi kabisa."
 
Yawezekana wasema kweli lakini ndio Dunia yetu ilivyo. Hakuna rais duniani anayewafaa wananchi wote. Yakitokea majanga upande wa pili husema "tuliyajua haya Hamkuona?" Iwe Baden, Ruto, Putin, Magu, au Mama Samia. Hoja yangu haihusiani na Uchaguzi..
 
Ndio maana nimetoa nafasi nanyi mtafakari na kutoa mawazo yenu. Huu ni ukumbi wa mijadala sio utafiti, au sio?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…