Chakula cha mchana shule za msingi ni kigezo kikubwa cha kuondoa utoro.

Chakula cha mchana shule za msingi ni kigezo kikubwa cha kuondoa utoro.

ligendayika

JF-Expert Member
Joined
Aug 31, 2012
Posts
1,183
Reaction score
198
Nimekua nitembelea shule za msingiWilaya ya Songea vijijini na kugundua kuwa shule zote zonazotoa chkula cha mchana zina mahudhurio mazuri ya wanafunzi na pia wanafunzi wake wanautayari mkubwa wa masomo hasa shule za kata za madaba na wino. Hata hivyo kata hizo pia zina wazazi ambao wana mwamko mkubwa juu ya elimu hivyo kuchangia chakula na michango mingine ya shule ni jambo la kawaida kwao. Swala kama hilo halipo katika kata nyingine hasa muhukuru ambako wananchi hawana mwamko wa elimu hivyo kutoona umuhimu wa kuchangia maswala ya elimu na utoro wa wanafunzi maeneo hayo ni mkubwa na ufauru wa kata hiyo ni wa chini. Naiomba serikari ilione hili na kuamua kuweka sheria ya wazazi kichangia chakula cha wanafunzi wa shule za msingi.
 
Mimi ni shuhuda! Nakumbuka kikombe cha uji mkavu (usio na sukari, chumvi au limao) ulikuwa kichocheo kikuu cha mahudhurio kwa Shule ya Msingi, pia ugali wa maharage (siku nyingine hayajaiva vizuri) vilitufanya tuhudhurie shule.
Yote kwa yote, wale wavivu katika masomo tulikuwa tunawakejeli kwa kuwaambia wanakuja shule kwa sababu ya uji (kwa Msingi) na ugali (kwa Sekondari). Hii ilisaidia kidogo wavivu kukaza msuli ili kupunguza kashfa.
Kama si kikombe cha uji mkavu, na ugali wa maharage.............
 
Shule zenu za kijijini hizo...weka mauji shuleni uone kama watoto wa dar watakuja shule hata uweke burger hawaji
 
Shule zenu za kijijini hizo...weka mauji shuleni uone kama watoto wa dar watakuja shule hata uweke burger hawaji

Mkuu TZ sio dar tu. Idadi ya shule dar haizidi shule za vijijini waelevu tulishaiondoa dar na matatizo ya TZ ndo mana kila kitu mnataka dar tunazungumzia shule za vijijini. Mind you dar kuna watoto waahitaji maharage hayo unayoyoponda.
 
Shule zenu za kijijini hizo...weka mauji shuleni uone kama watoto wa dar watakuja shule hata uweke burger hawaji

Kumbe kwa sasa Dar hakuna watoto wanaoshinda njaa shuleni!. Nashukuru Mungu huko Dar nimekaa na kujionea hali halisi (kwa kuwa mimi ni mdau wa Elimu). Acha sisi tuliosomea kijijini sitimbi, zama hizo kufika shule saa 12:30 asubuhi na kutoka ni saa 10:00 jioni tueleze ukweli.
 
Back
Top Bottom