Mkuu [USER=46913]gpblaze[/USER],..Mara nyingi mlo hutegemeana na kazi,(majukumu), wakati n.k. kwa watu wa "kawaida" yaani wale hufanya kazi mchana na kupumzika usiku. ni vizuri kutumia mlo huu.
Kutumia vyakula vya Protini zaidi na kuepuka vyakula vya Wanga, mafuta na kuepuka matunda mengi zaidi.Hii ni kwasababu kuna ongezeko/tokeo kubwa la sukari kutikana na matunda(Fructose) na wanga(Carbohydrate pia.Kwa kawaida Insulini inayotolewa mwilini hupungua kadiri muda wa siku unavyokwenda(yaani kupungua kuanzia asb hadi jioni- Insulin spikes) na hivyo basi vyakula vyenye Wanga na Sukari zaidi huweza kusababisha, kutolewa kwa Insulini tena na mmeng'enyo wa chakula kuwa mrefu na wakati mwingine kuingiliana na kuharibu usingizi.
Wengi huamka wachovu au husema "usingizi ule asubuhi asubuhi hivi ndiyo mtamu" ..hii ni kutokana na mwili(viungo vya mwili,hasa mfumo wa chakula) kufanya kazi usiku kucha(hasa kutokana na vyakula tajwa hapo juu) na wakati ule wa asubuhi mfumo kumaliza kazi yake na viungo vya mwili kuhitaji kupumzika baada ya kaxi ya usiku mzima lakini akili(mind) kukuhitaji kuamka kukabiliana na majukumu ya siku hiyo.