Chalamila anajitahidi lakini anapaswa kuongeza ustahimilivu wa kusikiliza

Chalamila anajitahidi lakini anapaswa kuongeza ustahimilivu wa kusikiliza

GoldDhahabu

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2023
Posts
7,189
Reaction score
10,375
1. Albert Chalamila ni Mwalimu kitaaluma, anafahamu kuwa kusikiliza ni mojawapo ya communication skills muhimu sana.

2. Mwananchi aliyelalamika watoto kubakwa anafahamu kituo cha Polisi kilipo. Aliamua kulalamika kwake badala ya Polisi kwa kuwa ana imani naye zaidi kuliko Polisi.

3. Kama alikuwa anaogopa kuwa taarifa mbaya kuuhusu mkoa wake zitafika mpaka Marekani, kwa nini alifanya mkutano mbele ya makamera?

4. Alichokifanya kinaweza kuwavunja moyo wananchi kuyatoa ya moyoni.

Labda alipaniki. Asilaumiwe. Ila anapaswa kujirekebisha.

Pamoja na mapungufu hayo machache, bado ni mmoja wa wakuu wa mikoa wachapa kazi nchini. Heri yake yeye alau anajitahidi hata kama bado hajaiva kwenye listening skills kuliko baadhi ya wenzake ambao wapo kama hawapo.

Hajamfikia Makonda lakini kajitahidi! Aboreshe tu uwezo wake kusikiliza.
 

Attachments

  • SIWEZI_KUKUCHEKEA_OCD_UKO_WAPI_WEWE_NTAKUBEBA_NIONDOKE_NA_WEWE_SAKATA_LA_MTOTO_KULAWITIWA....(...mp4
    11.7 MB
Yeye hata suit kaiweka kabatini hataki kuvaa vyuti wakati viongozi wenzake wanazipigilia suit
 
Back
Top Bottom