ChoiceVariable
JF-Expert Member
- May 23, 2017
- 66,537
- 75,687
My Take
Hii mikutano iwe inapelekwa Arusha na Zanzibar ndiko hakuna uhaba wa Hoteli,hapo Dar kumejaa ma Bar na Hoteli za Kawaida ambazo Hazina hadhi ya Kimataifa.
==
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kufanikisha mkutano wa wakuu wa nchi za Afrika kuhusu nishati, uliomalizika hivi karibuni mkoani humo.
Chalamila amekiri kujifunza mambo kadhaa baada ya kupokea wageni wengi Mkoa wa Dar es Salaam wakiwemo wakuu wa nchi za Afrika, akisema suala la usafi katika mkoa huo linawezekana huku akiahidi kuweka mikakati muhimu ya kuhakikisha mkoa huo unakuwa msafi kwa kipindi chote.
Hata hivyo amesema katika mapokezi ya wageni wa mkutano huo, miongoni mwa changamoto zilizojitokeza ni uchache wa hoteli.
Kufuatia changamoto hiyo Chalamilla amesena wiki ijayo itaundwa kamati maalumu itakayotembelea majengo chakavu na kushirikiana na wamiliki wa majengo hayo ili kuyaboresha na kuyafanya kuwa hoteli za kisasa.
Pia amegusia mpango wa Mkoa wa Dar es Salaam kuboresha na kuongeza uwekezaji katika maeneo ya vivutio ikiwa ni pamoja na Coco Beach ili kuwawezesha watu kutoka mataifa mbalimbalil kutembelea maeneo hayo.