Aramun
JF-Expert Member
- Nov 8, 2023
- 461
- 2,213
Naona kuna watu wanajaribu kutwist uhalisia wa mambo yalivyo mahospitalini kutokana na aliyoongea mkuu wa mkoa wa Dar, Mhe. Chalamila.
Ila huo ndiyo uhalisia wa mambo ulivyo kwenye mahospitali yote ya umma kuanzia dispensari mpaka hospitali ya taifa.
Zile huduma wanazohubiri wanasiasa kwamba ni bure ni uongo. Hakuna cha bure na mwananchi unatakiwa ulipie.
Ngoja niwape mifano midogo tu:
1. Wanasiasa huwa wanahubiri kwamba wazee wote miaka 60 na kuendelea wanatibiwa bure.
2. Vilevile watoto chini ya miaka 5 wanatibiwa bure.
Pia soma: RC Chalamila asema mjamzito anayegoma kununua gloves akajifungulie nyumbani. Hafai kuendelea kubaki madarakani
3. Wamama wajawazito nao wanasiasa wanadai wanatibiwa bure.
Ila uhalisia ni kwamba hayo makundi 3 hapo juu msamaha walionao ni gharama ya kufungua faili tu (Consultation fee) ndiyo hawalipii. Lakini gharama zingine zote ikiwemo vipimo, dawa na gharama ya kulazwa/kitanda wanalipia kama kawaida na wanalipa kwa kiwango kilekile kama wagonjwa wengine.
Muhimbili kwa sasa ukijifungua kawaida gharama yake ni 300,000/= na ukijifungua kwa operation gharama ni 700,000/=. Kumbuka hizo ni gharama za kujifungua tu tofauti na gharama zingine kama vipimo na dawa.
Hivyo kwa wale mnaopiga kelele Chalamila kakosea, hajakosea bali ameongea ukweli na uhalisia wa mambo yalivyo, tena mnapaswa mumshukuru kwa kutoboa siri.
Wanaotakiwa kuwajibishwa kwenye hili ni wanasiasa wengine ambao wamekuwa wakidanganya umma kwenye hili jambo, wakati uhalisia hauko hivyo.