Chalamila: Kwenye vyanzo vya maji Dar hatuna ukame tatizo kwenye mitambo ya kuchuja na kusukuma maji

Chalamila: Kwenye vyanzo vya maji Dar hatuna ukame tatizo kwenye mitambo ya kuchuja na kusukuma maji

Cute Wife

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2023
Posts
1,906
Reaction score
5,000
Wakuu salam,

Chalamila ameelezea kinachopelekea ukosefu wa maji kwa wakazi wa mkoa wa Dar katika ziara ya Majaliwa wilaya wa Temeke iliyoanza leo Oktoba 5, 2024.

"Mahitaji ya maji katika mkoa wa Dar kwa siku ni mita za ujazo laki sita na themanini na tano sawa na lita milioni sit ana themanini na tano, lakini uzalishaji wa maji kwa sasa upo kwenye mita za ujazo kama laki tano na thelathini na nane, hii inamaanisha tuna upungufu wa mita za ujazo kidogo na ndio maana baadhi ya maeneo kuna vilio vingi vya ukosefu maji.

Pia soma: Waziri Aweso akutana na DAWASA kwa lengo la kuboresha huduma ya maji katika Mkoa wa Dar es Salaam na Pwani

"Kule kwenye vyanzo vya maji yapo, hatuna ukame kabisa wa maji, kuyatoa maji kutoka kwenye chanzo ili yafike kwenye mtambo wa kuchuja maji na maji yaweze kusafirishwa kweda kwenye matenki pale ndio pana tatizo kidogo, mitambo ya kuchuja na kusukuma maji ndio matatizo kidogo nah apo sasa mitambo ile ndio inayopelekea uzalishaji wa maji usiwe mkubwa sana Kwenda kwa watu, na ndio maana mahitaji yanayohitajika kwa siku yanakuwa hayawezi kufikiwa kutokana na huo uchakavu kidogo ya hiyo mitambo."

 
Duh ,hawa wasaidizi wa rais Samia hakuna kitu kichwani,miaka 60 ya uhuru hatuna chujio la maji kwa wakazi wa mji unaochangia 30+ya pato la taifa

USSR
 
Back
Top Bottom