Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 12,699
- 22,598
Kuna ule usemi kwamba ukiwa na mtu ndani ya nyumba yako, akaamua kutumia rungu kuua mbu bila kujali mbu yuko sehemu gani. Sasa waswahili wanasema, kuna siku mbu anaweza kutua sehemu nyeti ya mwili, na muuaji mbu kwa rungu ataleta madhara makubwa!
Sasa naufananisha utendaji wa Chalamila na kauli zake na mtu anaeua mbu kwa rungu. Chalamila anaongea na kufanya mambo kwa namna ambayo mara nyinge inabidi ujiulize kama mtu aliyemteua haoni aibu (embarrassment) kuona na kusikia yale mteule wake akiongea au kufanya.
Tukianza na suala la dada poa, ametumia rungu kuvunja kila kitu kukiwa na matokea kwamba ameua mbu watatu lakini amevunja karibu nusu ya vyombo vya udongo ndani ya nyumba. Na hiyo haikutosha. Kwa kufuata mfano wako, DC wake na kaja kufanya mambo ya ajabu hadi kufikishwa mahakamani. Na wakati suala hili likiwa kwenye chaneli za kisheria, Chalamila anakuja kukazia kwamba alichofanya DC ni sahihi kabisa na kitaendelea! Hivi kuna akili zinatumika hapa kweli?
Haya, tuje kwenye suala la mgomo wa wafanyabiashara. Wakati mawaziri wakitafuta suluhisho la amani, Chalamila yeye kaenda kutoa vitisho na kusema anaweza kupeleka wanajeshi wawachakaze wafanya biashara Kariakoo kama wanavyofanya huko DRC! Chalamila anaongea utafikiri yeye ndio Amri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Tanzania, huku Rais na mkuu wa majeshi wanamsikiliza. Nashinda kuelewa hawa watu wawili walijisikiaje wakimsikiliza Chalamila anatoa vitisho kwa wafanyabiashara kwamba ana uwezo wa kuamrisha jeshi dhidi yao. Ni huyu Chalamila aliedai alishapiga risasi mwizi nyumbani kwake na kumuua lakini sijasikia akiitwa Polisi kuhojiwa juu ya jambo hili!
Sasa, mwisho wa yote, nimefikia mkataa kwamba Chalamila hafai kabisa kuwa kwenye uongozi wa jumuia ambao unamu-expose kwenye media. Labda apelekwe kuwa balozi wa Tanzania Rwanda au DRC huko au Gaza, kama tuna ubalozi huko, na kumuondoa kabisa katika safu ya uongozi wa wananchi nchini. Mie sioni Chalamila anafaa kazi gani nyingine, maana hii ya Mkuu wa Mkoa hafai kabisa. Kuna mambo mengi sana yanamharibikia Raisi Samia kwa sasa, na kuwa na watu kama Chalamila kwenye safu ya uongozi ndio wanaharibu hata zaidi.
Pia soma: