Cute Wife
JF-Expert Member
- Nov 17, 2023
- 1,906
- 5,000
Chalamila ameyasema hayo katika ufunguzi wa maonesho ya biashara Dar Saba Saba ambako Rais Nyusi wa Msumbiji alikuwa mgeni rasmi;
"Sisi wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam kama ambavyo tunayo hamu wewe kuendelea kuwa mkazi wa Dar es Salaam, usiende tena kuishi mkoa mwingine. Nitumie nafasi hii tena kumkaribisha kwa dhati Mh. Rais Nyusi na tunamuhakikishia kwamba Dar es Salaam ni mji salama na atapata kiwanja hapa Dar es Salaam, na tutamsimamia wakati wa ujenzi.
"Lakini pia nimeambiwa kule Zanzibar kama anahitaji kuwa na eneo la kujenga kiwanda atapata ule mkoa wa Kusini katika wilaya ya Kati katika kijiji cha Dungu ambako limeandaliwa eneo kubwa sana kwaajili ya masuala ya uwekezaji. Kwahiyo Mh. Nyusi tunakukaribisha sana, wala usiogope, Tanzania ni ya kwako."
Wakuu, kwani Rais wa nchi nyingine anaweza kupewa zawadi ya kiwanja kama hivi tena na Mkuu wa Mkoa?