Chalamila: Tukijenga desturi ya kutoza kodi hata kwenye biashara ndogo tutaepuka ukwepaji kodi

informer 06

Member
Joined
May 11, 2024
Posts
66
Reaction score
49
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila amesema malalamiko mengi ya kikodi utokea kutokana na kutojengwa kwa utamaduni ya watu kuanza kulipa kodi wakiwa katika ngazi za chini.

IMG_3851.jpeg
Akizungumza katika uzinduzi wa Kampeni ya Elimu kwa Umma na Upokeaji wa Malalamiko ya Kodi, inayoratibiwa na Ofisi ya Msuluhishi wa Malalamiko na Taarifa za Kodi ikiwa na kauli mbiu isemayo 'Kataa ukwepaji Kodi, kataa Kodi za dhuluma', Chalamila amesema kwamba kutegemea kumtoza kodi Mtu ambaye ajajengewa misingi tokea awali ni vigumu kuepuka mazingira ya kusuguana kwa kuwa wengi wanakuwa hawajajengewa utamaduni huo.

"Mimi kitu ambacho hamtonisikia nikiwa mfuasi nacho ni watu kutolipa kodi kutoka biashara hata ya 500, kwangu mimi ukiniuluza maoni yangu, mimi kama mwanataaluma wa kawaida maoni yangu mimi kodi lazima itolewe kwenye kila aina ya biashara, ndogo, ya kati au kubwa."amesema Chalamila

Amedai kutokana na mazingira ya utamaduni wa watu kutolipa Kodi imekuwa ikiwafanya baadhi kuwa wakwepa Kodi kwa njia mbalimbali, ambapo ametolea mfano wa baadhi ya wafanyakazi eneo la Kariakoo kujigeuza machinga ili wasitozwe kodi.

"Huwezi kuja kutengeneza (culture) utamaduni wa ulipaji kodi ukubwani .. na ndio maana leo huko Kariakoo watu wanajibadilisha wanakuwa machinga anajua akiwa machinga anaambiwa asilipe kodi"
IMG_3845.jpeg
Amesema kuwa utamaduni huo uchangia watu kudhani kwamba kodi ni suala la hiari badala ya kulitazama kama suala la lazima kwa maslahi mapana ya umma.

Pia ameeleza kuwa hata changamoto nyingi zinazoelekezwa kwenye ofisi ya usuluhishi anaamini kwamba zinatokana na uelewa, hivyo ujio wa kampeini hiyo unaweza kuchochea uelewa zaidi na kuondoa changamoto mbalimbali.

Ambapo amesisitiza "Uchangiaji wa maendeleo ya umma katika Taifa sio jambo la hiari kwenye mfumo huu wa Kodi ni mfumo wa lazima"

Hata hivyo ametoa ushauri kwa wasimamizi wa masuala ya kikodi kuona namna utaratibu wao wa kikodi unavyoweza kunyumbulika kulingana na hali au mazingira ya walipa kodi yanavybadilika kwenye nyakati tofauti.

Aidha Msuluhishi wa Malalamiko na Taarifa za Kodi, Erastus Vicent Mtui ametoa wito kwa jamii kujitokeza kupata elimu ambayo itawaepusha na malalamiko mbalimbali ambayo yamekuwa yakijitokeza hususani kwa wafanyabiashara.

Amesema kuwa ofisi ya Msuluishi wa malalamiko na taarifa za Kodi ilianzishwa kwa malengo mbalimbali ya kuleta usuluhishi ambapo majukumu yake ni pamoja na, kupokea malalamiko ya rushwa kwa maafisa wa kodi, kuupokea malalamiko dhidi ya matumizi ya nguvu kwa maafisa kodi, kupokea malalamiko ya kufungwa kwa biashara bila kuzingatia taratibu pamoja na malalamiko yanayoendana na hayo.

Katika uzinduzi wa kampeini hiyo ofisi hiyo imewakutanisha wadau mbalimbali ikiwemo viongozi wa wafanyabiashara kutoka mkoani Dar es Salaam, taasisi za kibiashara, wawakilishi kutoka kwenye vyombo vya ulinzi na usalama na watendaji wengine kutoka ofisini mbalimbali za Serikali na binafsi.

Kampeni hiyo ambayo imezinduliwa leo Juni 19,2024 katika viwanja vya Mnazi Mmoja inatarajiwa kuhitimishwa kwenye viwanja hivyo Juni 27, 2024, ambapo Mkuu wa Mkoa pamoja na wadau hao wametoa wito kwa wananchi hususani wafanyabiashara kujitokeza kupata uelewa na majawabu katika masuala mbalimbali.
 
⚖️Justice for Asimwe#
 
Chalamila vs Mwigulu
Chalamila" ...mimi kama mwanataaluma wa kawaida maoni yangu mimi kodi lazima itolewe kwenye kila aina ya biashara, ndogo, ya kati au kubwa."

Mwigulu" Siwezi kutafuta kodi kwa wafanyabiashara wadogo huku kuna wafanyabiashara wakubwa wanakwepa kodi"

Kati ya hao wawili nasimama na Chalamila, maoni yake ni yanahimiza ulipwaji wa kodi kwa lazima kwa kila mtu na suala la kulipa kodi ni la lazima.
 
Back
Top Bottom