Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 2,203
- 5,610
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Albert Chalamila amesema tayari bomoabomoa imeanza na inaendelea pembezoni mwa Mto Msimbazi ukianzia Jangwani ambapo amesisitiza kuwa zitabomolewa nyumba nyingi kwakuwa tayari Wakazi wengi wamelipwa fidia.
Akiongea Jijini Dar es salaam leo, Chalamila amesema “Tayari tumeshalipa zaidi ya Tsh. bilioni 50, Wananchi wanapisha mradi mkubwa wa uboreshaji wa kingo za Mto Msimbazi na ujenzi wa miundombinu ya kisasa”
“Wale wote ambao mmeshalipwa fidia msiende tena kujenga kwenye maeneo ya mabonde ambapo kesho mtavamiwa na maji na mwisho wa siku kuwa karaha na sio raha, tumieni fedha mlizopata kujenga kwenye maeneo mazuri, ambayo hayana migogoro”