serikali sikivu ya CCM itaendelea kutekeleza majukumu yake bila kujali chuki, mihemko au makasiriko ya mtu yeyote yule.Leo mmoja wa vijana aliyeongea na Mkuu wa mkoa wa DSM amemwambia wao wanaichukia serikali kuliko anavyoona mahala pale,
Kijana amekuwa mkweli, anaichukia serikali kwa sababu
Uwepo wa rushwa pale wanapotakiwa kushusha mizigo yaani unaingia Leo unashisaha baada ya siku nne kisa ujatoa rushwa hivi
Mh Chalamila nikuulize wale takukuru waliotangaza donge nono kwa watakao mkamata yule kengeza wa ccm yaani Msama promotion ndo wanao POKEA rushwa hapo Bandarini?
Mjinga sana huko serikalini mbona mishahara mingi ni hiyo hiyo 30k kwa siku. Ambayo ni sawa na 900kHakika vijana wanaichukia hii Serikali, hasa huyu Chalamila alishawahi kutamka hadharani vijana wanaoingiza tsh 30,000 kwa siku wasubiri kuolewa. Na hakuna hata tamko lolote la kukemea halijatoka. Wizara ya Vijana sijui waliichukuliaje hii kauli
Hawa wamelipwa ili kuichukia serikali.Akizungumza mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila hivi karibuni, Elias ametaja changamoto kadhaa zinazowasibu kwenye eneo hilo ikiwemo mrundikano wa mizigo mingi kupita uwezo, suala la rushwa na kukosekana kwa choo.
Mzungumzaji ni Elias Jonas Mwang'ingo ni Dereva wa Lori anayesubiri kupakia au kushusha mizigo katika Bandari Kavu iliyopo eneo la Mchicha Sandali, Temeke, Jijini Dar es Salaam
"Asilimia kubwa huku tunakoleta mizigo rushwa imetawala kwasababu unaweza kuona mtu anafika leo akaanza kushusha kwa sababu tu ametanguliza chochote kitu, lakini yule aliyemkuta ambaye anafuata utaratibu akashusha nje ya wakati" -Elias
"Sisi hapa watu wote ukiangalia tunaichukia sana serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, tunaichukia kwasababu watendaji wengi wa serikali wanajikumbatia wao, na sisi wengine ni kama vile hatuhusiki na hii Nchi" -Elias