Cute Wife
JF-Expert Member
- Nov 17, 2023
- 1,906
- 5,000
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa ipo, mlipaswa kuja hapa kwa kuwa ndio tunaolisimamia na siyo huko mlikokwenda," amesema Chalamila.Wafanyabiashara hao zaidi ya 800 jana Alhamisi Julai 11, 2024, waliandamana kutoka Uwanja wa Mnazi Mmoja kwenda ofisi za CCM Lumumba, kupinga kuondolewa kwa wafanyabiashara waliokuwa sokoni hapo kabla halijaungua Julai 2021.
Pia soma: DC Ilala awatuliza wafanyabiashara Kariakoo, kukutana na Chalamila kesho
Walichukua uamuzi huo baada ya kupinga utaratibu Shirika la Masoko Kariakoo kutenga siku tatu kuanzia jana kuhakiki majina yao ambao hawapo kati ya yale yaliyotangazwa.
Mara baada ya kufika ofisi hizo za CCM kufikisha ujumbe hao, viongozi wa chama hicho tawala waliwaeleza watulie baada ya kuwa wanaimba nyimbo mbalimbali na kufunga barabara.