BWANKU M BWANKU
JF-Expert Member
- Jan 12, 2019
- 377
- 435
Wote mnakumbuka kwenye Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2022 Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze iliyopo mkoani Pwani ilishinda na kuongoza Kitaifa katika Halmashauri zilizofanya vizuri katika ubora wa utekelezaji na usimamizi wa miradi ya maendeleo iliyotembelewa na Mwenge wa Uhuru.
Mwaka huu 2024, Chalinze imeendeleza wimbi la kushinda katika ubora wa miradi na usimamizi ambapo mwaka huu 2024 kwenye Mbio za Mwenge Halmashauri ya Chalinze imeibuka mshindi wa kwanza kikanda katika kanda ya 4 kwa ubora wa miradi. Chalinze imepokea kombe la ushindi kutoka kwa Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kwenye Kilele cha Mbio za Mwenge wa Uh mwaka 2024 Mwanza.
Halmashauri hii inaongozwa na Mkurugenzi wa Halmashauri Ndugu Ramadhani Possi na Mbunge wake wa Jimbo akiwa ni Mhe. Ridhiwani Kikwete ambaye pia ni Waziri katika Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu.