Challenge ya 2011; matches na results


thanks
 
tuombe mtoto wa mkulima ndio awe mgeni wa heshima fainali jamani tujitahidini juu ya hili

sidhani kama atakubali, yaani kuna asilimia kubwa sana kuwa yeye ndio atakuwa mgeni rasmi hasa ukizingatia kuwa timu ya nyumbani ndio imeingia final
 
Niko na wewe mwanangu, Poulsen is a real coach, sio mbabaishaji. Uzee dawa, huyu jamaa kazeekea kwenye soka anajua nini na wapi kitu kifanyike. Naamini Kilimanjaro Stars na Taifa Stars ya awamu yake itakuwa bora zaidi ya Maximo. Wakati utatudhibitishia ili.
 
Kwa kuwa Ivaory Coast ni wageni waalikwa kwenye mashindano haya hivyo basi hata kama watatufunga, sisi ndiyo tutakabidhiwa kombe kwa lugha nyingine sisi ni mabigwa tayari au nakosea wakuu....
 
Kwa kuwa Ivaory Coast ni wageni waalikwa kwenye mashindano haya hivyo basi hata kama watatufunga, sisi ndiyo tutakabidhiwa kombe kwa lugha nyingine sisi ni mabigwa tayari au nakosea wakuu....

nami nilikuwa najiuliza hilo swali ila sijapata jibu, maana kama waalikwa wakishinda itakuaje
 
Kwani waalikwa hawaruhusiwi kuchukua kombe wakishinda?
ina maana fainali ilikuwa jana? Jamani ulio karibu na CECAFA tupeni jibu tusherehekee kabisa. Tukisubiri fainali halafu tufungwe tutakosa raha
 
Kwa kuwa Ivaory Coast ni wageni waalikwa kwenye mashindano haya hivyo basi hata kama watatufunga, sisi ndiyo tutakabidhiwa kombe kwa lugha nyingine sisi ni mabigwa tayari au nakosea wakuu....
Nilisoma kitu kama iko kwenye gazeti siku za nyuma, wageni ( Zambia, Malawi, na Ivory Coast) hata wakishinda awachukui kombe. Ila ujue kuna kombe na pe$a. Kombe awapewi ila pe$a watapewa. Hivyo Kilimanjaro Stars ikishinda, itapewa kombe na pe$a. Lakini kama mgeni akishinda atapewa pesa tu.
 

Mkuu,
Safari hii timu alikwa ikishinda itapewa pesa ($ 30,000) plus replica ya kombe...
 
Mkuu,
Safari hii timu alikwa ikishinda itapewa pesa ($ 30,000) plus replica ya kombe...

Penati ya Tony Maweja iliyodakwa kiustadi na kipa Juma Kaseja iliisaidia timu ya taifa ya Tanzania Bara'Kilimanjaro Stars' kutinga fainali ya Kombe la Chalenji baada ya kushinda kwa penati 5-4 katika mechi yao ya nusu fainali dhidi ya Uganda kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam jana.
Stars waliokuwa wakicheza kwa kujituma zaidi jana na kutengeneza nafasi kadhaa za kufunga katika kipindi cha pili, walisimama imara dhidi ya mabingwa watetezi Uganda na hatimaye kumaliza dakika 90 za kwanza kwa sare ya 0-0.
Kabla ya kumalizika kwa dakika za kawaida, Stars timu zote zilifanya mashambulizi kadhaa ya hatari, zikiwemo walizokosa Stars kupitia kwa Mrisho Ngassa katika dakika ya tatu na dakika ya 70 huku Uganda wakikumbukia nafasi ya wazi ya dakika ya 49 wakati mpira wa kichwa wa Mike Serumanga ulipopanguliwa na Kaseja.
Dakika 30 za nyongeza hazikutoa mshindi na ndipo ikafikia hatua ya kupigiana penati ‘tano-tano', ambapo Stars iling'ara baada ya wachezaji wake kufunga penati zote kwa ufundi, huku kipa Kaseja akiwapa raha zaidi Watanzania na kurahisisha ushindi baada ya kuokoa penati ya nne.
Kipa Odongkara Robert wa Uganda alishindwa kudaka penati zilizojaa wavuni za nahodha Shadrack Nsajigwa, Stephano Mwasika, Shaaban Nditi, Salum Machaku na Erasto Nyoni.
Penati nne za Uganda zilifungwa na Isinde Isaac, Walusimbi Godfrey, Emmanuel Okwi na Andrew Mwesigwa.
Kutokana na ushindi huo, Stars wamefanikiwa kulibakisha kombe la Chalenji nchini, kwani wanafainali wenzao, timu ya Ivory Coast ambayo ilishinda 1-0 katika nusu fainali ya kwanza dhidi ya Ethiopia jana, si wanachama wa shirikisho la soka la Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) na wanashiriki wakiwa ni waalikwa, kama walivyokuwa wenzao wa timu ya taifa ya Zambia.
Hata hivyo, kama Ivory Coast watashinda dhidi ya Stars, watakabidhiwa zawadi ya mshindi wa kwanza ya kitita cha dola za Marekani 30,000 na Stars watakabidhiwa kombe la ubingwa wa mwaka huu.
FAINALI KIINGILIO SH 1,000

source:ippmedia
 
Kombe tayari tumeshalichukua kuanzia jana kwahiyo kesho ni heshima na kuzitafuta USD 30,000....Hongera Kilimanjaro Stars kwa kazi ya jana
 
Hivi kwani TFF mechi ya Taifa Stars na Brazil kiingilio hawakufanya 1000
 
Waganda wangetufunga jana wangeongea sana maana wangekuwa wametula kidude mdogo mtu na kaka mtu
 
Hivi kwani TFF mechi ya Taifa Stars na Brazil kiingilio hawakufanya 1000
kwanza tamaa na pili ukifanya kiingilio 1000 kwenye mechi kubwa kama hiyo watu watajaa utakosa pakuwa weka tatu kulikuwa na garama za kuwa leta brazil kama sikosei ilikuwa siyo chini ya bil 3...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…