Chama cha Kutetea Abiria (CHAKUA)

Chama cha Kutetea Abiria (CHAKUA)

Mgombezi

JF-Expert Member
Joined
Mar 23, 2009
Posts
610
Reaction score
181
Kwa mara ya kwanza leo nimepata kusikia kwamba kuna chama cha kutetea abiria pale ambapo mwenyekiti wake alipokuwa anahojiwa TBC1 katika kipindi cha usiku wa habari, alikuwa anahojiwa juu ya tukio la jana (1/5/11) madereva wa mabasi ya kwenda mkoani kugoma.

Swali langu ni kwamba chama hiki kimeanza jana tu au kipo muda mrefu, kama kipo muda mrefu siku zote wako wapi katika kuwaelimisha wananchi juu ya haki na wajibu wa abiria?

Hivi vyama vya utetezi vina dhamira ya dhati kweli katika kuwafikia wananchi au wanatafuta njia za kutoka kimaisha kupitia matatizo ya watu.

Naomba kuwakilisha!
 
Sijawahi kukisikia hata siku moja na kama siku zote kipo je huwa kinafanya kazi gani! ofisi zake zipo wapi? na contact zao zipo wapi ili iwe rahisi kwa abiria kuwapigia!

Umefika wakati sasa wa Media kufanya kazi zao ili kuboresha sharing na kurusha habari kama vyanzo vya information. Kutwa tunaona matangazo (billboards) za biashara tu mabarabarani ila vitu muhimu kama hivi hawabadiki sasa sijui mwananchi atajuaje sijui! aaaahh!

Wiki kabla ya easter pale Ubungo niliona mama mmoja kasukumwa na konda aisee akaumiza pelvis yake yule mama! halafu naanza kumsaidia eti kakataa nisimpeleke hospital au hata kumuadhibu yule kijana na kumpeleka polisi. Wananchi wamekuwa hawajui haki zao na wameshakata tamaa za maisha!
 
Hapa tz utaanzisha utitiri wa vyama na hutafanya chochote, cha msingi ni nchi kuwa na vyombo vyake vinavyo fuata ethics: wako wapi polisi au sumatra mpaka itokee enjio ya mfukoni imtetee abiria?

Ukienda kwenye mashirika makubwa ya ndege utakuta flyer inayokuelekeza haki zako kama msafiri na wajibu wa airline iwapo utaahirishiwa safari yako.

Huu utitiri wa taasis bibafsi zisizo na meno ni matokeo ya mmomonyoko wa ethics kwa taasisza uma zilikabidhiwa dhamana ya kumlinda raia.
 
Kuna mwenye taarifa zaidi juu ya chama hiki, nimejaribu kutuma email kwa huyu mwenyekiti lakini sikupata majibu, email yenyewe alisema chakuatz@yahoo.com au ni msanii fulani wa mjin?
 
Back
Top Bottom