Uchaguzi 2020 Chama cha Maaskofu chataka haki Uchaguzi Mkuu

Uchaguzi 2020 Chama cha Maaskofu chataka haki Uchaguzi Mkuu

beth

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
3,880
Reaction score
6,368
Chama cha Maaskofu na Wachungaji (TPA) kimeiomba Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kusimamia Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2020, kwa kuzingatia sheria, kanuni na miongozo ili haki itendeke.

Kimesema usimamizi wa sheria, kanuni, taratibu na miongozo kuhusu uchaguzi utasababisha vyama vyote kupata haki stahili na hivyo, kuondoa malalamiko ambayo yamekuwa yakijitokeza uchaguzi unapowadia na wakati mwingine kukaribia kutishia amani ya nchi.

Rais wa TPA, Askofu Musa Mlawi, alitoa rai hiyo wakati akizungumza na waumini kutoka madhehebu mbalimbali ya dini katika kongamano la kitaifa la maombi lililofanyika jijini Dodoma.

Mlawi alisema Watanzania wanatarajia kuona Tume ya Taifa ya Uchaguzi inasimamia haki na kufuata sheria, miongozo, kanuni na taratibu za uchjaguzi ili kuepuka malalamiko yanayoanza kujitokeza.

Aliwahakikishia Watanzania kuwa, Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu utafanyika mwaka huu utakuwa huru na haki, licha ya kuwapo dosari ndogo ndogo zinazojitokeza.

Alisema chama hicho kinaamini kwa asilimia zote kuwa uchaguzi huo utakuwa wa haki na huru, kutokana na watanzania walio wengi wamekuwa waaminifu kwa kuuombea mbele za Mungu kwa uaminifu.

Kwa mujibu wa Askofu Mlawi, kutokana na upendo wa Watanzania kuombea uchaguzi huu, chama hicho cha maaskofu na wachungaji kinaamini utafanyika kwa amani na taifa litapa viongozi ambao ni chaguo la Mungu.

Aliwataka Watanzania wenye vitambulisho vya kupigia kura, kutimiza haki yao ya kimsingi kwa kujitokeza kupiga kura ili kuwachagua viongozi wanaowataka kwa manufaa ya taifa.

Wakati huo huo: Askofu Mlawi ameipongeza Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais John magufuli kwa kuboresha miundombinu mbalimbali na kuimarisha uhusiano kati ya serikali na viongozi wa dini nchini.
 
Chama cha Maaskofu na Wachungaji (TPA) kimeiomba Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kusimamia Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2020, kwa kuzingatia sheria, kanuni na miongozo ili haki itendeke
Haki haiombwi! Haki inadaiwa. Hawa ni maaskofu njaa, wajasilia dini! Toa kauli thabiti kuwa NEC inawalazimu kutenda haki na si OMBI! Si hisani ya NEC kutenda haki, ni wajbu na LAZIMA, washinikizwe watende haki
 
Wanasemaje kuhusu uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka Jana?
Utawala ni ule ule afu wanatarajia haki!
 
Paragraph yako ya mwisho nimeinukuu imejitosheleza.

Wakati huo huo: Askofu Mlawi ameipongeza Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais John magufuli kwa kuboresha miundombinu mbalimbali na kuimarisha uhusiano kati ya serikali na viongozi wa dini nchini.

Asante sana
Queen Esther
 
Rais wa TPA, Askofu Musa Mlawi, alitoa rai hiyo wakati akizungumza na waumini kutoka madhehebu mbalimbali ya dini katika kongamano la kitaifa la maombi lililofanyika jijini Dodoma.
Rubbish! Maombi, kuna vitu vingine maombi hayasaidii, ni ujinga tu! Maombi wakati umepanda juu ya mti unataka kujiachia halafu unapiga maombi eti usiumie au kufa! Kwenye case kama hiyo hakuna maombi, ukipanda juu ya mti mrefu, au 20 storey building ukaruka na kutua kwenye mwamba utakufa tu , hakuna cha maombi hapo!
Pumbavu kabisa, Maaskofu na Mapasta waliikimbia Corona, hawakwenda kumwekea mikono mgonjwa hata mmoja leo wanaleta mipua yao eti kuomba!
 
Wakurugenzi walitolewa kauli kali sana.

"Nakupa Kazi.
Nakupa posho.
Nakupa mshahara.
Nakupa Nyumba
Nakupa Gari

Alafu unakwenda kumtangaza mpinzani Utakiona cha moto".

Hakuna mtu hata mmoja aliyeweza kukemea kauli hii ya kidikteta na machafuko kwa nchi.

Kwaheri jiwe kwaheri CCM.
 
Sijaelewa alichokisema Askofu.

Yaani uchaguzi utakuwa huru na wa haki wakati mchakato wote umegubikwa na uvunjifu wa haki ?
 
Naomba kwanza kuwajua signatories wa hiki Tamko. Maana maaskofu wa awamu hii ya fly over kusema kweli wanastahili kupanda majukwaani tu kama mameneja kampeni ijulikane moja
 
Hiyo paragraph ya mwisho ndio kwenye maudhui makuu ya huu uharo wa askofu njaa mlawi,pumba.ff zake
 
Kuna kikundi cha watu chenyewe kinahubiria amani tu kuelekea uchaguzi mkuu, mambo ya haki wao hayawahusu.
 
Baada ya askofu Mwamakula kujitokeza kuunga mkono haki, ndo mnaanza kuchomoka kutoka mafichoni.....haishangazi siku hizi mahubiri yenu yanahusu zaidi utoaji wa sadaka, bisheni...
 
Mgogoro utaanzia hapa, mawakala wa upinzani hawataapishwa na wakurugenzi, na wakiapishwa hawataruhusiwa kuingia kwenye vituo vya kupigia kura.wakiruhusiwa kuingia kwenye vituo watanyimwa fomu za matokeo. Upande wa vijijini chadema wakizembea kuweka mawakala huko ndo vituo vingi feki vitaongezeka...
 
Hiko chama kina usajili? Je usajilia wake ulo hai? Wanakaguliwa? Hao Maaskofuna Wachungaji wana vyeti? Wamesomea wapi? Chama kimekaguliwa mahesabu yake? 😎
 
Mbona awamu hii ya 5 kuna vyama maajabuajabu sana ambavyo havikuwahi kuwepo
 
Back
Top Bottom