amirmojaElimu
New Member
- Nov 23, 2024
- 1
- 0
Kwa hivi karibuni kila Mtanganyika na Mzanzibari ameshuhudia Serikali inayoongozwa na CCM ikiwa ni kinara wa kuendelea kuwasahaulisha kizazi hichi kipya historia mama ya Nchi yao Iliyo ni tunda la Muungano yaani Tanzania.
Sherehe za Uhuru wa Tanganyika zimekuwa kama ni hisani, hazipewi kabisa kipaumbele cha kulinda historia hii adhimu.
Ukiendelea kustaajabu ya Tanganyika kwa Tanzania utayaona CCM Kupitia Website ya Chama Cha Mapinduzi ccm.or.tz
Yenye kutoa historia na utambulisho wa wapi wametoka na wapi wana kwenda.
Ni aibu mfumo wa Tehama wa chama kama CCM kutuambia kuwa Mwenyekiti wa ASP AfroShirazParty aliluwa ni Sheikh Aman Abeid Karume (Rais wa Zanzibar Awamu ya 6)
Kwa minajiri hio ina mtaja kama Ndiye Kinara pia wa Mapinduzi za Zanzibar huku ikimtupilia mbali Ndugu Sheikh Abeid Amani Karume(Raisi wa kwanza Serikali ya Mapinduzi Zanzibar SMZ) ambaye ndiye muhusika wa historia hii adhimu.
CCM kama haina Team yenye weledi katika masuala ya tehama basi tuendelee kuvuna haya mauza uza na upotezaji wa kumbukumbu wa kutisha kiwango hichi.
CCM na tehama kwao ni kama Uchawi na Teknolojia Uwoga na uzito ni mkubwa kuliko uhalisiaa.
Wanatutia aibu na kutuaibisha kama nchi maana hawawezi kabisa kusoma na hata kuandika.
Mfikishieni Taarifa Mwenezi Makala na Yule Bashite Mwendawazimu wa Arusha na Mtangulizi wake Pale Lumumba ofisini