SI KWELI PreGE2025 Chama cha Mapinduzi kimetoa orodha ya majina 10 ya awali ya Wagombea, wamo Ole Sabaya, Makonda na Hersi Said

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Chama cha Mapinduzi kimetoa orodha ya majina 10 ya awali ya Wagombea, wamo Ole Sabaya, Tulia Ackson na Hersi Said

​
 
Tunachokijua
Madai
Julai 21, 2025 imeibuka barua yenye utambulisho wa Chama cha Mapinduzi ikionesha orodha ya wagombea 10 walipita kwenye hatua ya awali kakita mchakato wa kipata wagombea wa ubunge ndani ya chama hicho unaoendelea.

Uhalisia wa madai hayo
JamiiCheck imefuatilia taarifa hiyo na kujiridhisha kuwa si ya kweli na haijatolewa na chama cha mapinduzi (CCM).

Ufuatiliaji umebaini kuwa Taarifa hiyo haijachapishwa wala kutolewa na CCM kama inavyoonekana. Kupitia kurasa zao rasmi za mitandao ya kijamii CCM hawajachapisha taarifa hiyo.

Taarifa hiyo kwa Umma ni ya kughushi kwani Taarifa kwa umma zinazotolewa na CCM zina QR code ambayo inamuwezesha mtu ku scan na kupata taarifa hiyo kwa njia ya PDF lakini taarifa hiyo inayosambazwa QR code yake imehaririwa na hivyo kushindwa kutambulika kwa urahisi.

Aidha Katibu wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa, itikadi, uenezi na mafunzo Amos Makalla alizungumza na waandishi wa habari Julai 19, 2025 ambapo alibainisha kuwa mchakato wa kuwapata wagombea wa nafasi ya ubunge na udiwani umesogezwa mbele hadi Julai 28, 2025 na hivyo watu waendelee kuwa watulivu.
Hahahahahahaaa!! Wanasikilizia upepo unakwendaje?
Kazi ni kipimo cha utu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…