Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
Barua hiyo hapo chini inajieleza inakotoka na kichwa cha habari ndiyo hicho.
Wanafunzi watakuwa na safari ya kutembelea magofu ya kale Kunduchi na kujifunza historia ya utumwa na historia ya Waarabu waliotawala Pwani ya Kunduchi.
Si tabu kuelewa watakachoelezwa vijana wetu kwani historia hii ni maarufu hakuna asiyeijua.
Ushauri wangu ni kuwa katika ratiba hiyo yao waongeza na kulizuru kaburi la Mzee Mshume Kiyate ambae kazikwa Kunduchi kwenye makaburi ya kale.
Wawaonyeshe vijana wetu kaburi la Mzee Mshume Kiyate na waeleze historia yake na mchango wake katika kupigania uhuru wa Tanganyika akiwa bega kwa bega na Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere hadi uhuru kupatikana mwaka wa 1961.
Naamini historia hii ni muhimu katika kujenga uzalendo kwa hawa vijana wetu wadogo kuliko propaganda za Waarabu na Utumwa.
Historia ya Waarabu na Utumwa inafahamika.
Historia isiyofahamika ni hii ya Mzee Kiyate Mshume.