Chama cha Soka Afrika liangalieni hili.

bryan2

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2016
Posts
3,323
Reaction score
4,679
Chama cha Soka Afrika (CaF) inabidi waliangalie hili kwa jicho la pili na kulifanyia mabadiliko kama wanataka kwenda na Sayansi ya Mpira.

Hapa nazungumzia haya mashindano mawili kombe la Mabingwa Afrika na Kombe la shirikisho Afrika kwa kifupi hii michuano imepoteza mvuto tofauti na kipindi cha Nyuma au kulinganisha na Michuano ya Mabara Mengine ngazi ya vilabu.

La Kwanza CAF inabidi wajitangaze sana na kutafuta udhamini mnono zaidi ili ligi hizi ziwe na mvuto tena na bahati nzuri siku hizi kuna chombo kimoja cha habari kinaonyesha hii michuano Mubashara tofauti na Supersport lakini huezi kuta wakifuatilia mfano bingwa wa Kombe la Mabingwa mwaka huu Wydad Athletic Club ya Morroco baada ya kumfunga Al ahly ya Egypt wengi wetu tu hatuijui na hata humu JF Sikuona habari zozote kuhusu michezo hii Siku ya fainali hii inaonesha ni jinsi gani Caf hawatoi matangazo ya kutosha.Pia kutakua na mchezo wa Fainali kati ya Tp Mazembe na Supersports ya Afrika kusini ila mpaka sasa hakuna matangazo yoyote kuitangaza fainali hizi,hapa inabidi Caf kitengo cha Masoko na habari wajitangaze sana.

Na pili ligi fainali ya ligi hizi imekua ikichezwa kwa mfumo wa ugenini na nyumbani hili nalo naona halijakaa vizuri Caf wangetafuta Kiwanja kimoja either hata uwanja wa Taifa hapa Bongo or Kasarani pale Kenya na Kwingineko na Fainali kupigwa moja tu,hili litaongoa zile dhana kuwa timu ikiwa nyumbani inabebwa na kushuhudiwa na watu tofauti na kufanya watu wengi zaidi kuifuatilia.

Kazi kwenu Caf.
 
Ndio maana simba hatunaga mpango na hayo mashindano tumeyapuuza kitambo tumeamua bora tu tuwe tunambamiza chura wa majini na kufurahisha nafsi zetu baasi....CAF wakitaka turejee tena kwenye mashindano hayo basi wajirekebishe
 
Kuhusu FAINALI kupigwa ktk NEUTRAL GROUND kwa upande wa Africa ni gumu!

Pata picha Fainali ya waarabu watupu ipelekwe pale TAIFA, kwa waafrica tulivo, ule uwanja utabaki mweupe! Hiyo italeta taswira hasi kwa ulimwengu! Kampuni gani za udhamini au Tv ziko tayari kuonyesha Mechi ya uwanja empty?

Kwa kukuongezea tu, uefa wanafanya utafiti kuona kama mfumo wa HOME - AWAY UEFA FINAL utaongeza Economic benefits, nao wautumie!
 
Ndio maana simba hatunaga mpango na hayo mashindano tumeyapuuza kitambo tumeamua bora tu tuwe tunambamiza chura wa majini na kufurahisha nafsi zetu baasi....CAF wakitaka turejee tena kwenye mashindano hayo basi wajirekebishe
Duh ! Kuna watu ni jeuri mpaka basi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…