Pdidy
JF-Expert Member
- Nov 22, 2007
- 57,951
- 32,619
Na Zulfa Mfinanga, Bariadi
CHAMA cha United Democratic Party (UDP) wilayani Bariadi mkoani Shinyanga kimepata ushindi wa kishindo dhidi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika kinyanganyiro cha kugombea nafasi ya makamu mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya hiyo.
UDP imepata ushindi huo kufuatia uchaguzi uliofanyika hivi karibini wa
kumpata makamu mwenyekiti wa halmashauri hiyo, baada ya baraza la madiwani kuamua kufanya mabadiliko ya nafasi hiyo na kumuondoa aliyekuwa akishikilia nafasi hiyo, Eliakimu Sudi.
Baraza hilo la madiwani lilifikia uamuzi huo hivi karibuni katika vikao vyake na hatimaye kuteua wagombea na CCM ilitoa mgombea wake Getruda Ngokolo na UDP ilimteua Benjamin Stephen .
Katika kinyanganyiro hicho, CCM ilipata kura 15 huku UDP ikiibuka kwa kura 19 na jumla ya kura zote zilizopigwa ni 34. Msimamizi katika uchaguzi huo, alikuwa mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo, Deogratias Hela.
Diwani aliyeshinda katika kinyanganyiro hicho ni kutoka katika Kata ya Nyakabindi kupitia tiketi ya UDP ambaye sasa atakuwa makamu mwenyekiti wa halmashauri hiyo wakati Mwenyekiti ni Peter Matondo ambaye ni wa UDP.
Naye Ummy Muya anaripoti kuwa Diwanai wa Kata ya Makuburi katika Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, Busee Ji-gabhas ameiita Manispaa ya Kinondoni kuacha kupiga porojo za siasa na badala yake wawajibike katika kuboresha sekta mbalimbali hususan sekta ya elimu ambayo bado inalega lega.
Ji-gabhas alisema hayo jana katika kikao cha baraza la madiwani la Manispaa hiyo wakati akitoa hoja kuhusu wakaguzi wa wizara ya elimu kuruhusu shule kufunguliwa wakati hazina maji wala vyoo.
Alisema kwa mfano shule ya Sekondari Makoka ambayo hivi sasa inajulikana Charles Keenja sekondari, wanafunzi katika shule hiyo, wanatumia mawe na maji kujisafisha baada ya haja kubwa.
Naomba hili liangaliwe tusisubiri mpaka Waziri Mkuu au Waziri wa elimu afike ndipo tuanze kutupiana lawama kwamba madiwani hatuwajibiki ipasavyo kiutendaji, manispaa inatakiwa ijibane katika bajeti yake ili kutatua tatizo hilo,alishauri.
Akichangia hoja hiyo inayoilenga kamati ya uchumi, afya na elimu mbunge wa jimbo la Ubungo Charles Keenja alisema Manispaa imeelekeza nguvu zaidi kwenye elimu ya sekondari wakati kuna shule za msingi za siku nyingi ambako wanafunzi wamerundikana madarasani.
Shule ya msingi Mzimuni, Makulumla na nyingine nying
zina ufinyu wa madarasa, hakuna hata vyo, ni tatizo hivyo tusiende mbele tukasahau nyuma,alisema Keenja.
Mwenyekiti wa Kamati ya Uchumi, Afya na Elimu, Hashim Mbonde alisema kuna vikwazo vingi vinavyo ikabili sekta ya afya kama vile kuchelewa kupata dawa kutoka bohari kuu na kwamba vifaa vinavyotolewa na idara ya kuhifadhi madawa (MSD) ni vibovu.
Alisema katika mwaka wa fedha 2009/10 tatizo la maji mashuleni litakwisha kabisa kwa kuwa tayari wamewasiliana na Mamlaka ya Maji Safi (Dawasa) ambao walieleza asilimia 75 ya mtandao wa maji katika Wilaya hiyo, uko salama isipokuwa Bunju,Mbweni na Goba.