Chama cha ujamaa na kujitegemea cuk(self reliance and socialist party SSP) na dhamira yake ya gawio la Rasilimali KWA kila mwananchi!je itawezekana!!?

Mwl Athumani Ramadhani

JF-Expert Member
Joined
Sep 10, 2022
Posts
1,280
Reaction score
2,522
Baada ya katiba mpya kupatikana hiki ni Moja ya chama kitakacho sajiliwa kikiwa na dhamira njema ya kurudisha nguvu ya umma kwenye rasilimali zetu yaani wananchi wapate gawio la Moja KWA Moja la rasilimali zao kupitia akaunti za Benki na simu zao.

Wadau wa uchumi mnadhani ndoto hiyo inaweza kutimia kwamba KILA Mwezi mwananchi wa kawaida apate gawio la Rasilimali zilizopo kutokana na uwekezaji unaoendelea kufanywa kwenye migodi,Mbuga za wanyama na vivutio mbali mbali vya utalii!!?

Tunaomba mchango wenu katika hilo tupate pa kuanzia,Sijawahi kusikika hili jambo tangu kuanzisha KWA Taifa hili!Tuna dhamira ya dhati kabisa kuhakikisha KILA mtanzania anafaidika Moja KWA Moja na rasilimali hizi huko mbeleni KWA kupata gawio la Moja KWA Moja ambalo litamsaidia kujikimu kimaisha kama nchi zilizoendelea zinavojali Hali ya Maisha ya wa Hali ya chini.

Sisi kama wajamaa wa kisasa tuna lengo la kulifanya jeshi la magereza na jkt kama kitovu kikuu cha uchumi wa nchi yetu KWA kuanzia kwenye kilimo,usafirishaji wa bidhaa na abiria na VIWANDA kama ifuatavyo;-

KILIMO NA MIFUGO

Serikali yetu itatenga maeneo makubwa ya kilimo na ufugaji,kilimo cha mazao ya chakula na biashara pamoja na usindikaji wake Ili kudhibiti mfumuko wa bei za vyakula kama mafuta ya kula!tutakuwa na maduka ya vyakula ya umma!bidhaa zote zitatoka VIWANDA vya serikali Ili kudhibiti mfumuko wa bei kutoka sekta Binafsi.

Jeshi la magereza na jkt ndio wazalishaji wakuu na kitovu kikuu cha uchumi wetu!tutajenga makambi mashambani na wataishi huko huko kama wazalishaji wakuu!kesi za mahabusu zitaharakishwa Ili kupata nguvu kazi na vijana WENGI waliomaliza darasa la saba na kidato cha nne watajiunga na jkt na kutumika KWA miaka kumi mfululizo Ili kulitumikia nchi yao !na sera hii itapunguza idadi ya wahuni mtaani!

Maziwa,nyama na bidhaa nyingi zitazalishwa KWA wingi ili kuwafikia watumiaji kirahisi na KWA bei nafuu mfumuko wa bei utaisha,pia serikali itapata mapato mengi kuliko kutegemea Tozo na kodi pekee!tutashirikiana na sekta binafsi katika uuzwaji wa bidhaa hasa machinga na wenye mitaji mikubwa!


UCHUKUZI NA USAFIRISHAJI

Vyombo vya usafiri vya serikali vitachuana na sekta binafsi Ili kuleta tija kwa wasafiri kuanzia boda boda,bajaji,dala dala,malori na mabasi yatachuana vilivyo na sekta binafsi Ili kudhibiti mfumuko wa bei za nauli kiholela holela!!

Hayo ni baadhi ya malengo makuu ya chama chetu Baada ya katiba kupatikana !tumeona sekta Binafsi pekee imeshindwa kuwa msaada na kuwa mnyonyaji wa wananchi.

Wakati wa kurudi kwenye misingi ya uwajibikaji umefika!

Tunaomba mchango wenu kufanikisha azma na ndoto hii kutimia kwa nchi yangu Tanzania.

"Mzee Warioba ajumuishwe kwenye kikosi kazi cha mkandala mchakato wa katiba mpya ukamilike"
 
hatuwezi kuiacha sekta Binafsi PEKEE iamue hatma ya wananchi wetu!!

Sekta binafsi imefeli Sana lazima ipewe ushindani na serikali Ili kuleta huduma bora KWA WANANCHI!!

Wakati umefika !!

Sekta binafsi itashindanaje na serikali wakati serikali ina nguvu ya dola na inatunga sheria ambazo sekta binafsi inabidi izifuate? Halafu sekta binafsi ndiyo inalipa kodi wakati serikali inatumia hiyo kodi halafu warudi kushindana. Hayo yatakuwa ni mashindano kweli?
 
Serikali ndio imefeli ndio imekwamisha sekta binafsi isikue. Mfano kupitia kodi. Importations tax ni kikwazo cha ukuaji uchumi.
 
Tatizo la nchi hii ni kuporomoka kwa Hofu ya Mungu kwa watu wake wakiwemo wanao tuongoza. Matokeo yake ni kuporomoka kwa maadili katika jamii yote. Mwizi na fisadi wanaheshimiwa na kuhusudiwa na jamii. Wewe fikiria serikali inapeleka mswaada Bungeni bila hata soni wa kutaka kuwajengea wauza unga mahabusu zao. Hizi mahabusu zitumike kuhamasisha wale punda wabebaji aka moles usiwe na wasiwasi kwani hutafungwa hata ukikamatwa na wakati unasubiri tukutetee hata mahabusu utakuwa zile spesheli kwa wauza mihadarati tu.
 
Unaporuhusu magari kuingia nchi bila kodi utakusanya kodi nyingi Sana kuliko ukiweka kodi kwa magari yanayoagizwa. Faida yake
1.Utashawishi watu kumiliki magari sababu yatakuwa bei ndogo. Wakishamiliki tu magari ndipo unapokuja wabamizia kwenye mafuta, bima, fine, parking, garage, spareparts, ushuru wa stand,sumatra fee,ukaguzi fee,fire fee,unawapiga na ushuru wa barabara, cheap to import but expensive to run.
 
Mbona mnarudi kule kule walipofeli kina Mwalimu
Ujamaa wa kisasa hautokuwa sawa na wa Mwalimu !kutokana na mahitaji ya Zama hizi!sisi tutakaa meza Moja na sekta binafsi na kuleta mstakabali ulio sawa KWA WANANCHI wetu!hatutoiua sekta Binafsi bali tutaiboresha ili ilete tija kwa jamii!

Mfano leo wafanyabiashara wa mafuta wanatesa wananchi KWA kujipanga bei wanayotaka sisi kama chama na serikali tutashusha bei kuwa ya Kati yenye maslahi KWA wananchi yaani ujamaa wetu utakuwa regulator wa sekta binafsi kutowaumiza wananchi!!

Tutajikita katika ujasusi wa uchumi na sio tu ujasusi wa kushika dola ambao umetamalaki tangu Uhuru!!!
 
Wazo ni zuri Ila mnatakiwa kufanya “Hybrid Socialism”.
 
Ni sumu kuanzisha chama cha kijamaa chenye 100% “Pure Socialism”.
 
Pendekezo chama inabidi kitumie “ Meritocracy system ”. ili kupata viongozi bora na sio bora viongozi.

Viongozi watakao kuwa tayari kulinda falsafa za chama na kutanguliza maslahi ya taifa mbele kuliko yao.
 
1. Chama kitaanza lini ?

2. Mchakato wa kukusanya wanachama una anza lini ?na utafanyikaje ?

3. Falsafa za chama zitatungwa na wanachama wote au viongozi tu ?
 
1. Chama kitaanza lini ?

2. Mchakato wa kukusanya wanachama una anza lini ?na utafanyikaje ?

3. Falsafa za chama zitatungwa na wanachama wote au viongozi tu ?
Baada ya katiba Mpya kupatikana mkuu!!

Katiba ikishapatikana tu yote yatawekwa wazi!!

Tusubiri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…