Chama cha Waagizaji na Wasambazaji wa Mafuta Tanzania (TAOMAC) chakanusha uwepo wa sintofahamu kati yake na EWURA

benzemah

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2014
Posts
1,533
Reaction score
3,187

Tumebaini kuwepo kwa taarifa kwenye baadhi ya mitandao ya kijamii ikidai kuwa waagizaji na wasambazaji wa mafuta wamekaa kwenye kikao na EWURA na kuishia kwenye mtafaruku na kutokukubaliana.

Kwa niaba ya Wanachama wetu wa Chama cha Waagizaji na Wasambazaji wa Mafuta Tanzania (TAOMAC) ambao wanajumuisha zaidi ya 97% ya soko la mafuta yanayoingizwa nchini, tunapenda kukanusha taarifa hizi kwa kuwa sio za kweli.

Hatujaakaa kikao na EWURA kwa zaidi ya wiki mbili. Pia hatujawahi kukaa kikao na EWURA na kuishia kwa mtafaruku.

Aidha, sekta ya uagizaji na usambazaji wa Mafuta inapitia changamoto ya Ukosefu wa Dola, lakini tumeshakaa vikao na mamlaka zinazohusika na tumeahisiwa kuwa tatizo hili linafanyiwa ufumbuzi.

Wanachama wetu wanaendelea kuagiza mafuta na wataendelea kufanya hivyo ili hakikisha nchi haikosi Mafuta.

Pia soma: DOKEZO - Kashfa ya Rushwa na Uhaba wa Mafuta: Hatma ya EWURA na Waagizaji wa Mafuta
 
Jana nimepita petrol station zaidi ya tatu mkoa wa songwe hawana petrol- sijui shida ni nini?
 
Siku chache nyuma kuna mtu aliwaponda majirani kwa kukosa dola eti kwetu imejaa tooooop kiko wap sasa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…