Chama cha Waganga wa Tiba Asilia Simiyu, wakana chama chao kujaa makada wa CCM

Chama cha Waganga wa Tiba Asilia Simiyu, wakana chama chao kujaa makada wa CCM

KwetuKwanza

Member
Joined
Mar 13, 2023
Posts
82
Reaction score
150
Mara baada ya kuibuka maneno mengi mitaani kuwa Chama cha Waganga wa Tiba Asilia na Tiba Mbadala Mkoa wa Simiyu kina makada wengi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Mwenyekiti wa umoja huo, Mayunga Kidoyai amefafanua kuwa taaluma yao au kazi ya mtu binafsi haiwezi kuingiliana na suala la kichama kwa kuwa ni vitu viwili tofauti.

Akifafanua juu ya uongozi wa chama chake ambao umeingia madarakani katika uchaguzi uliofanyika Machi 12, 2023 na kutakiwa kuongoza chama hicho kwa kipindi cha miaka mitano, amesema:

“Madai kuwa chama chetu kimekuwa cha siasa, niweke wazi tu Tanzania kama Nchi haina dini ila kila Mtanzania ana imani yake.

“Sekta hii ninayoongoza mimi haina usiasa ila kila mmoja ana mapenzi yake binafsi kwa kuwa pale ni hospitali, daktari wa pale anaweza kumtibu mtu yeyote bila kujali nafasi ya ukada wake.

“Ndani ya chama chetu tunapokuwa katika suala la kazi hatuwezi kukataa kumtibu mtu kwa kuwa ni kada wa chama fulani, nenda kasome hata kwenye kanuni za chama, kuwa kwenye chama hakukuzuii kuwa na kazi nyingine.

“Ukimkuta mtu anazunguzia habari za uganga kwenye masuala ya chama anapotosha kwa kuwa ni vitu vinavyotofautiana, pia sisi katika idara yetu tumepelekwa Serikalini kupitia Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii…”

“Hata sisi Waganga kuna muda tunaonewa na Serikali, wanakuja kututisha hivi na vile, lengo ni apewe hela, ndio maana tunakuwa na uongozi wa chama ili tuwe na njia sahihi.

“Pia utambue kuwa vyeo vya kisiasa ni vya muda lakini upande wa pili nina ajira yangu na nina taaluma yangu ambayo ninaweza kuzikwa nayo.

“Mfano Katibu wangu wa Mkoa ni CHADEMA, hapo unadhani kuna ukada hapo?”

Chama hicho kimekuwa kikituhumiwa kujihusisha zaidi na masuala la siasa kutokana na viongozi wake wengi kuwa wanasiasa, ambapo Mwenyekiti wake ni Katibu Umoja wa Vijana Wilaya ya Kwimba Mkoani Mwanza, Makamu wake ni Diwani wa CCM katika Wilaya ya Meatu Mkoani Simiyu huku mlezi wa chama hicho akiwa Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Simiyu Shemsa Mohamed.
 
Back
Top Bottom