Tetesi: Chama cha wakulima Tanzania (TASO) chapokwa kuratibu sherehe za nane nane

Tetesi: Chama cha wakulima Tanzania (TASO) chapokwa kuratibu sherehe za nane nane

Tembo2

JF-Expert Member
Joined
Jan 1, 2014
Posts
510
Reaction score
858
603f53601dc8c89795d2c811e7084c25.jpg


Sherehe za wafanyakazi (Mei mosi) zinasimamiwa na vyama vya wafanyakazi zikiratibiwa na TUCTA.
Sherehe za wafanyabiashara sabasaba zinaratibiwa na TANTRED NA TCCIA.
Sherehe za wakulima (wakulima, wafugaji na wavuvi) zinaratibiwa na TASO
Mh.Raisi/ waziri mkuu upo uvumi ulionea na uliotangazwa na katibu mkuu wizara ya kilimo,ufugaji na ushirika kwamba chama cha TASO kimefutwa na maadhimisho ya sherehe ya wakulima (NANENANE) ziratibiwe na watumishi (sekretarieti za mikoa).Kwa nini Mh.Raisi/waziri mkuu kama chama cha TASO kimefutwa kwa nini sherehe za nanenane zisifutwe?kuliko kusimamiwa na wasiohusika.
Sisi wanachama wa TASO tumesikitishwa sana na jambo hili kwani hatuelewi chama chetu kimefutwa kwa taratibu zipi,mbona hatujashirikishwa kupitia vikao vyetu kwa mujibu wa KATIBA ?
Pamoja nakuwepo au kutokuwepo jambo hili hivi vyama vya wafanyakazi vikifutwa TASO Au TANTRED wanaweza kuratibu nakusimamia sherehe za wafanyakazi?.Kinachotusikitisha zaidi hao watumishi wa UMMA walioteuliwa kuratibu nakusimamia wana WELEDI kiasi gani na shughuli za wakulima?
Mh Raisi/waziri mkuu sisi wakulima ambao ndio kundi kubwa nchini tunanyanyasika sana na hawa watumishi wa UMMA ambao hujiona kwamba wana WELEDI mkubwa kuliko sisi wakulima kama ambavyo msajili wa vyama hiari (mambo ya ndani)alivyoamua kwa makusudi kutofuata taratibu nakufuta chama chetu bila kutushirikisha kwakua sisi ni mambumbumbu kama wanavyotuita kitendo ambacho tunakilaumu sana .Mh .Rais/Waziri mkuu hawa sekretarieti zamikoa wametupangia viingilio vikubwa kuingia kwenye viwanja ambavyo ni mali yetu TASO mfano kiingilio uwanjani mtu mzima Tshs 2000/ na mtoto 1000/ hivi Mh tunaenda kufanya biashara au kujifunza mbona wenzetu wafanya kazi wanapopeleka matatizo yao kwako huingia bure?uwanjani?


Jambo jingine ni kwamba sisi TASO tulikua tunatoa kiingilio kidogo kupata pesa zakuendesha chama je hizi sekretarieti za mikoa hizo fedha watakazokusanya wanapeleka wapi?
Jingine Mh .hawa watumishi walioteuliwa kuratibu shughuli za NANENANE wametoka kwenye vituo vya kazi takribani mwezi kuanzia tarehe 01/07/-9/8/2012 je wananchi wanapata wapi huduma zao na kauli mbiu ya awamu ya TANO ni HAPA KAZI TU,sasa kusimamia sherehe za nanenane ni kazi inayowalipa mishahara na huku wanalipwa posho kila siku je nisahihi.


Tunafikisha kilio chetu kwako juu ya swala hili kwani wewe ndio Mkombozi Wetu wakulima tumechoka kunyanyasika hasa katika awamu ya Utawala wako.

Post sent using JamiiForums mobile app
 
Labda maudhui ya sherehe hayaendani na madhumini ya TASO. Lakini pia chama cha wafanyakazi kuwa tegemezi kwa serikali sio kkitu kizuri. Mwanzoni nilifikiri hivi viwanja vya NaneNane vinamilikiwa na TASO kwa kutumia Hati za Kumiliki ardhi, kumbe hali iko tofauti. Kama ingekuwa eneo ni lenu na serikali imewapoka kungekuwa na mushkeli.
 
TASO waache ubabaishaji. Ni wapigaji wazuri.Nimeona maonesho ya hapa Arusha yapo vizuri pia Jeshi LA Polisi linasimamia vizuri. Ila hiyo sekreatariat itoe tathmini ya mapesa baada ya maonesho

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkome...ninyi si ndo uwa mnaongoza kuvaa YANGA....
 
Back
Top Bottom