Chama cha Walimu (CWT) special thread

MWALIMU DAIMA

Senior Member
Joined
Mar 4, 2023
Posts
129
Reaction score
263
Habari wakuu, hope wote ni wazima.
Pasi na kupoteza muda ni ende kwenye lengo la Uzi huu.

Awali yoyote mm ni mwanafunzi wa shahada ya kwanza ya ualimu katika moja ya chuo kikuu apa Tanzania mwaka wa pili.

Napenda kushauri na kutoa mawazo Yangu kuwa, ni Wakati sasa walimu kwa kushirikana na serikali kufuta Chama Cha walimu Tanzania yaani CWT, kwani kumekuwa na malalamiko mengi sana kuwa chama hiki hakipo kwa ajiri ya maslahi ya walimu.

๐Ÿ“Œ๐Ÿ“Œ Kipi kifanyike baada ya kufutwa kwa chama hiki๐Ÿ“Œ๐Ÿ“Œ

Nashauri baada ya chama hiki kufutwa, ni Wakati sasa wa kuanzisha vyama vya walimu kwa kutegemea na masomo yao.

Yaan kuwe na chama Cha walimu wa masomo ya Sanaa, chama Cha walimu wa masomo ya sayansi, chama Cha walimu wa masomo ya biashara.

Ni faida ya kuwepo kwa vyama hivyo

01. Itasaidia walimu wa masomo husika kutambua changamoto zao specifically, na kuja na solution ya changamoto zao kwa kushirikiana na serikali na washika dau mbalimbali

02. Itasaidia walimu wa masomo husika, kuhusika moja kwa moja kikamilifu katika suala la uandaaji wa mitaala kulingana na msomo yao

03. Itapunguza work overload ambayo Ilikuwa inafanywa na cwt kwan Kila walimu watakuwa na sehemu yao specific

04. Pia itasaidia uanzishwaji wa bank za walimu kutokana na masomo yao, yaani Kila walimu na masomo yao wawe na benki yao mfano benki ya walimu wa masomo ya sayansi.

๐Ÿ“Œ๐Ÿ“Œ๐Ÿ“Œ๐Ÿ“ŒJe utaratibu wa uongozi utakuwa vip???๐Ÿ“Œ๐Ÿ“Œ๐Ÿ“Œ
Nashaur kuwa uongozi, uwe Free from government, yaani Kila chama kijitegemee ki sera, kiuchumi na kiutawala,

๐Ÿ“Œ Kwanini kiuchumi, Kila mwalimu atakuwa anafanya contribution kwa chama chake husika kutokana na makubaliano yatakayo weka๐Ÿ“Œ


@ Nakupenda Tanzania, mm ni mwalimu daima @

 
Ewe mwalimu! Kwa nini kisivunjwe jumla na kisianzishwe kingine chochote??
 
Hiyo CWT ni ๐Ÿšฎ tu.

Haijawahi kuwa na msaada wa maana kwa wanachama wake. Imagine mwalimu anakatwa kila mwezi 2% ya mshahara wake, halafu akistaafu bila hata chembe ya aibu, eti wanampa bati 20!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ