Chama cha walimu hatukitaki

sigitoro

Member
Joined
Oct 13, 2012
Posts
68
Reaction score
6
Nikiwa kama mmoja wapo wa walimu wa Tanzania nimefanya uchunguzi asilimia kubwa ya walimu hawakitaki hicho chama kwasababu kiko kwa maslai ya wakubwa na serikali.Sasa kuendelea kutushinikiz kujiunga mnatafuta kuongez matatizo ktk sekta ya elimu.N:B WAZIRI WA ELIMU WALIMU TUNASEMA CHAMA CHA WALIMU HATUKITAKI NAJUA UNAWEZA KUWATETEA LKN WEWE UKO HUKO JUU UNAKULA UPEPO TU NA SISI HUKU CHINI NDY TUNATESEKA,TUNASEMA HATUKITAKI
 
Wasipop[igana mwaka huu tukaongezewa maslahi tuliyoyadai bc tunawato wote kwenye uongozi.
 
Mkuu sawa,lakin kwanini walimu kama wafanyakaz wasiwe na chama chao? lakini kwanini serikali isitusikilize walimu?
 
Na bado serikali na chama chao cha walimu kama hawatusikiliz 2tawaonyesha.picha ndy kwanza linaanza
 
Katika Dunia ya leo hakuna mfanyakazi anayejitetea mwenyewe. Vyama vya wafanyakazi vilikuwepo enzi na enzi na matunda yake yanajulikana dunia nzima.
Mimi sio mwalimu lakini ni mdau wa CWT.
Walimu mnahitaji kutoa maoni yao kwa viongozi husika na kuelezea matatizo yao na viongozi wanawajibu wa kuyatatua.
Tanzania kumekuwa na historia ndefu katika vyama vya wafanyakazi, hakijawahi kutokea chama chenye muono wa maendeleo kama CWT na kwa uelekeo huo ni lazima kipigwe vita hasa na wadau wa serikali ambayo ndiyo mwajiri

Chama cha walimu kina vitegauchumi vifuatavyo:
1. Mwalimu house DSM
2. Ofisi za mikoa 21 ambazo ni maghorofa yasiyopungua gharama za Tshs 350,000,000/=
3. Wana zaidi ya Tshs 10Bilioni kwa ajili ya kuanzisha Benki ya Walimu
4. Wanajiandaa kujenga jengo la benki ya Mwalimu DSM Manzese
5. Ni chama ambacho makatibu wakuu ambao ni watendaji wilaya zote Tanzania na Mikoa yote Tanzania wana magari ya
kufanyia kazi.

Nafikiri hakuna chama hata vya Siasa Tanzania Ukiondoa CCM chenye uwezo wa pekee kiuchumi kama CWT

Ni wajibu wa walimu kuelezea wanataka nini kuboresha mahitaji yao kwa viongozi wa CWT . Benki itakapo anzishwa walimu wote utakuwa ndio mwisho kukopa kwenye mabenki mengine kwa riba wanayotaka wao. Waungeni mkono benki ianze muanze kuonja matunda ya umoja wenu.

Kungekuwa na vyama Vitatu kama CWT masilahi ya wafanyakazi Tanzania yasingenyonywa na wanasiasa ambao wanajijali wenyewe. Mishahara inapanda bungeni watendaji makazini wanaumia.

Mwalimu jipe Moyo hii ni vita na lazima mshinde.
 
Mkuu kweli bila CWT mambo hayaendi maana wabunge wamebaki kupigania uccm na uchadema.
 

akijibu swali lililoulizwa na mbunge machali kuhusu walimu kutaka kujitoa kwenye cwt,waziri gaudensia kabaka amesema kwa kuwa walimu waliojiunga na cwt wanazidi nusu ya walimu wote hivyo sheria zinazohusu vyama vya wafanyakazi inawalazimu kuwakata hizo asilimia 2 kwa lazima wale wote ambao bado hawajajiunga na cwt.
Huu ni uonevu unaofanywa na cwt wakishirikiana na serikali dhaifu.
Walimu wote tuungane dhidi ya hila hizi kwa kuwashinikiza mukoba na timu yake wajiuzulu nafasi zao na cwt ifumuliwe na kuundwa upya ili kiwe chombo imara chenye misimamo yake na kipiganie haki za walimu wote.
Mapambano yanaendelea
 
Hv cwt inamsaidiaje mwalimu maana mi nashindwa kuelewa!Walimu wamekuwa wakinyanyaswa na serikali yao mishahara midogo,posho za mazingira magumu hakuna,nyumba za walimu mashuleni hakuna!Mwalimu anapostaafu hathaminiwi kabisa na cwt hasaidiwi kitu chochote na chama chake!CWT wekeni mikakati ya mizuri ya kusaidia walimu wake na pia kuwathamini walimu wastaafu!
 
Miradi ya maghorofa inamsaidiaje mwalimu wa bujugo? acheni mawazo mgando walimu tuitoeni CWT na tunakomaa na mgomo wetu.
 
Yaan wengne hata fomu hatujajaza tayar wanakata 2% juu kwa juu, huu n ubabe uliopitiliza, itaendelea kuwa 3*3 = 33, mpaka tupewe teachng allwance km wabunge wanavyopata stting allwance per day!
 
wote hapo juu mnao tetea CWT naona ndy mnakula mishahara yetu.
1.Mpk leo kuna walimu wapya hawajapata mishahar yao mmewasaidia vp? kama c kusubiri wakianza kupewa 2 muuanze kukata pesa yao WALIMU TUKATAE HIKI CHAMA.
2.Walimu wapya 2mefika kuripot hakuna mkataba wowote ambao tumewekeana na CWT waanze kukata pesa yangu wao wanakata kwa mkataba upi? kama c unyonyaji
3.Kama mlizoea kuwaliza walimu wa zamani.basi ni hao hao ujio wa walimu wa sasa ni reasonable sana.
4.Kujiunga na hicho chama chenu hatutaki kulazimishwa.
5.Mashuleni hatutaki sura zenu..

N:B WALIMU WA ZAMANI NA SASA NI TOFAUTI 2NAOMBA MUELEWE TUKO PROFFENSIONAL ZAIDI TUNAUELEWA KULIKO MNAVYOFIKIRIA.
 
WALIMU MNADHALILISHANA WENYEWE, mimi nilikuwa mwl, ni katika fani nzuri sana kufanya kazi, kama uonavyo watu wengi wakitamani kuingia bungeni wapate mishahara mikubwa, tena kwa kujipangia wenyewe ni Bunge, Mprof, Dr, na wataalamu wengi wameingia kule wakitumia usomi wao kama waalimu wa zamani. Prof maana yake ni kuwa ktk taasisi ya elimu ajenge taaluma, lkn kwa shida zinazoikumba elumu ya Tanzania wataaluma wengi wameikimbia fani hiyo.

Chama cha walimu kilipashwa kutetea maisha ya mwl lkn wanakuwa kama sukari inapanda na kushuka, presha inapanda inashuka, wanakosa credibility kuitwa viongozi wa chama. Walimu ni wapole sana, lakini MTAKE MSITAKE wanasikitika matokeo mabaya ya f4-2012 lakini wanachekea moyoni wakisema serikali na mwalimu mjanja au mhuni nani. mwl na serikali wanavutana sana chini kwa chini. Serikali ama bila kujijua ama wakijua wanakiachia chama cha walimu cwt kikiwaburuta walimu
1.benk
2. mwl house project
3.nk

walimu wanafaidika na nini?

mwalimu lazima aamke mwenyewe, ingawa wapo ambao wameamua kuchukua hatua kuingia ktk NGO, Walimu wengi sana wenye uwezo mkubwa sana wamehshamia katika miradi mbali mbali, hata HAKIELIMU wapo, nk
 
Mkuu kweli bila CWT mambo hayaendi maana wabunge wamebaki kupigania uccm na uchadema.

cwt hamna cha maana.mapendekezo yapo tele lakini hakuna anayejali.tusidanganyane cwt kipo kisiasa zaidi na hakipo kuhakikisha maslai ya walimu.cwt ipo kama bakwata(kugandamiza haki za waislamu) huku zenyewe zikijifanya zina uchungu.cwt ni biashara ya vigogo!
 
Dawa ya kuondokana na adhabu ya ualimu ni kusoma kwa kubadili fani au kufanya plan B yeyote i.e kutotegemea kufundisha peke ake.CWT hamna watakachofanya cha maana.narudia cwt kipo kisiasa zaidi
 
Ni kweli kuwa CWT imepiga hatua kwa kutaja hayo mali. lakini walimu wanataka kujua mwalimu ananufaika vipi na hiyo mali. wengine wamechangia cwt miaka na dahari na sasa wanastaafu bila kuondoka na chochote kutoka chama.hiki cama kimekuwa sawa na baba mwenye mali, magari nk. lakini watoto hawajawahi hata kupewa lifti. walimu wananufaika zaidi na Saccos kuliko CWT. sasa uandaliwe utaratibu mzuri namna kila mwalimu anavoweza kunufaika mfano kutibiwa, masomo, huduma za kisheria, makazi na wakati wa kustaafu. pia umilikaji wa rasilimali zake kama benki uwe ni wa walimu kwa zaini ya nusu na walimu wapate gawio kutokana na faida. kusiwe na cwt na halafu walimu bali walimu wawe ndo cwt.
 

like mkuu
 

Sasa mwalimu ananufaika vp na hayo maendeleo, hata mikopo 2 wameshindwa kuwapa walimu,madai yao wameshindwa kuyatetea.na wewe ni mwizi 2 coz sio mwalimu lakini unajifanya mdau wizi m2pu, tena umenikera pimbi wewe,sasa subirini moto unawaka muda sio mrefu mtakoma wapuuzi nyie.
 
chama cha walimu kuwanacho si vibaya sana endapo kinaendeshwa kwa uwazi but kuna ifisadi mkubwa ndani yake ambayo walimu wengi sasa wameshakidungua, vinginevyo kifanyiwe reformation kuhusu vipi mwalimu mmoja mmoja anafaidik na mchango wake anaokatwa kila mwezi mgogoro mkubwa uko hapo, lakini pia viongozi waliopo ni corruptive sana kwenye maslahi ya walimu hawasimami na walimu. hata mimi naunga mkono hoja kwa asilimia zisizopungua mia1
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…