Chama cha walimu na maslahi ya Mwalimu

Chama cha walimu na maslahi ya Mwalimu

Mwl Philemon

Member
Joined
Nov 29, 2018
Posts
63
Reaction score
70
download (1).jpeg


CWT ni chama cha walimu kama kinavyojipambanua na kujitangaza siku zote za uwepo wake. Zaidi kinatangazika kwa sifa ya kutetea maslahi ya Mwalimu, haki na kumpigania mwalimu ili apate mazingira mazuri ya kazi.

Nafikiri imefika wakati sasa kama chama kijitathmini hasa kuhusu kazi yake na gharama kubwa anayotozwa Mwalimu kukihudumia chama kuliko chama kinavyompatia mwalimu huduma.
Kuna mambo matatu napendekeza yafanyike katika chama chetu ili kuleta msawazo na kupunguza manung'uniko miongoni mwetu.

Mambo hayo ni haya hapa

1. Mwanachama achangie mara moja tu kwa mwaka na vitegauchumi na michango itakayopatikana vitumike kukiendesha chama kwa mwaka husika.
2. Viongozi wa chama kwa ngazi zote wawe walimu wenyewe ili kusiwe na mishahara kwa watumishi wa chama bali zibaki posho tu wakati wa vikao na utekelezaji wa majukumu ya msingi ya chama.
3. Chama kiwe na akaunti page zinazokuwa na usimamizi mzuri kwa ajili ya kupokea na kujibu maoni na changamoto za wanachama wake. Hii itasaidia kupunguza vikao pia.
Umefika wakati cha kuondoa mzigo mkubwa kwa mwalimu. Hati ya mwalimu ni lazima makato yapungue sasa.

Tusiimbe tu solidarity wakati wachache mnakula vizuri wengine mnaachana maumivu mioyoni mwetu.
download.jpeg
Asilimia 2% ni kubwa sana. Kama kweli chama kina upendo na mwalimu ni bora asilimia 1% ipelekwe NHIF ili mwalimu ahudumiwe kikamilifu kuhusu afya yake na wategemezi wake.

Walimu wanalalamika mazingira magumu ya kazi halafu viongozi mpo kimya mnaendelea kupambana kuua vyama vingine bila kuchukua hatua za kumsaidia mwanachama wenu. Mnaendelea kugawana pesa yake na kufurahia na familia zenu.

Makato ya asilimia 2 yafike mwisho sasa.
Dada yetu Ester kabla hatujaenda kwenye uchaguzi wa mwaka kesho tafadhali sana simamia kupunguza makato haya. Asante sana.
 
Back
Top Bottom