Chama cha walimu, ukweli ni upi?

blackice2100

JF-Expert Member
Joined
May 11, 2020
Posts
2,188
Reaction score
2,897
Nimekuwa muumini sana wa kusoma magazeti kila siku kujua yanayojili ijapokuwa nilichobaini waandishi wengi ni wanafki wakubwa walioamua kuiacha kalamu yao na kufuata upepo wa kisiasa!

Habari zao ni za kutabirika na za mezani zaidi kuliko za kuzitafuta na kwa sasa ni za kumpamba mtawala aliyeko madarakani japo naamini ni za kinafki kama kawaida yao.

Ngoja Samia aondoke madarakani ndo utaiona rangi ya hawa wanafki walioamua kukimbia taaluma yao na kuwa wapiga debe wa kusoma upepo.

Ngoja niingie kwenye hoja ya msingi; Hebu naomba kujuzwa mmiliki wa hili gazeti haswa ni nani la Jamvi la Habari?

Hili gazeti kama si kwa makusudi basi kuna mtu ana ajenda zake za kugombanisha viongozi wa WALIMU na SERIKALI tena anatumia nguvu kubwa sana sijajua ana maslahi gani.

Nakumbuka tangu wale viongozi walipoomba kutohudumu nafasi walizoteuliwa na Rais mama Samia yaani hili gazeti limekomaa na hawa watu haswa.

Hebu wapana wa maarifa mtufungue macho kuna nini nyuma ya pazia?
 
Laana ya Pesa za walimu itawaua mwa nyie.


Hapa unalalamika kama juha.
 
Laana ya Pesa za walimu itawaua mwa nyie.


Hapa unalalamika kama juha.
Binafsi wala siyo mwalimu na wala sijihusishi na mambo yao ila naona kama hiki chama kimeandamwa sana tangu wale viongozi kuomba kutenguliwa kwa nafasi zao na kibaya zaidi kuna gazeti linatumia nguvu kubwa sana kuhakikisha wale viongozi wanaondoka CWT sijajua kuna nini nyuma ya pazia chief!!!
 
Basi achana na mambo yasiyokuhusu.

Wanaokatwa 2% ya mishahara yao kila mwezi kushibisha matumbo ya hao wezi ndio wanajua maumivu yao.

Kwa taarifa anayekata mishahara ya watumishi na kuwapa CWT ni MWAJIRI ambaye ndio huyo huyo serikali.
 
Hiki chama ni kikoba kinachonufaisha viongozi majizi...
 
Kwani shida iko wapi hasa kwa hilo gazeti kuamua kupambana na hao viongozi wezi wa fedha za walimu!
 
Basi achana na mambo yasiyokuhusu.

Wanaokatwa 2% ya mishahara yao kila mwezi kushibisha matumbo ya hao wezi ndio wanajua maumivu yao.

Kwa taarifa anayekata mishahara ya watumishi na kuwapa CWT ni MWAJIRI ambaye ndio huyo huyo serikali.
Ila hilo ni la siku mingi,,,, cjajua kwanini hawa walioko sasa wanashambuliwa sana baada ya kuonyesha misimamo flani,,,,, anyway ya NGOswe acha tumuachie NGOswe but nilitamani kujua kilichoko nyuma ya pazia baada ya kuona Jamvi La Habari limewashupalia hawa viongozi!!!
Mmiliki wa Jamvi La Habari ni nani na amelikomalia hili katika mlengo UPI?! Ndicho nilichohtaji kupata mwanga
 
HAKUNA msimamamo wowote.

CCM, SERIKALI na CWT/Vyama vya wafanyakazi wote lakwao ni moja.

Wala usidanganyike
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…