Chama cha Wanasheria Tanganyika chaendesha Mafunzo juu ya haki ya uhuru wa kujieleza

Chama cha Wanasheria Tanganyika chaendesha Mafunzo juu ya haki ya uhuru wa kujieleza

Pfizer

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2021
Posts
590
Reaction score
807
Chama cha Wanasheria Tanganyika (The Tanganyika Law Society - TLS) imeendesha mafunzo ya kuwajengea uwezo asasi za kiraia toka sahemu mbalimbali nchini juu ya haki ya uhuru wa kujieleza ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa majukumu yake kwa umma.

Mafunzo hayo yamefanyika tarehe 20 Mei 2024 jijini Dodoma.

Wahudhuriaji wa Mafunzo hayo, Wameeleza Umuhimu wa Uhuru wa kujieleza na wajibu wake.

Wahudhuriaji wamesema Uhuru wa kujieleza ni ule ambao hauvunji haki za mtu mwingine wala hauendi kinyume na Sheria za Nchi. Wameelezea kwamba unaweza kujieleza kwa kuongea, kupiga kelele za kuomba msaada, kuchora au kuandika.

Kwenye Katiba ambayo ni ibara ya 18 inaeleza vizuri sana ambavyo Mtu anaweza akatumia haki hii ya kujieleza.

Haki ya Uhuru wa Mawazo (Ib 18)

18. Uhuru wa Maoni

(1) Bila ya kuathiri sheria za nchi, kila mtu yuko huru kuwa na maoni yoyote na kutoa nje mawazo yake, na kutafuta, kupokea na kutoa habari na dhana zozote kupitia chombo chochote bila ya kujali mipaka ya nchi, na pia ana uhuru wa kutoingiliwa kati mawasiliano yake.

(2) Kila raia anayo haki ya kupewa taarifa wakati wote kuhusu matukio mbalimbali nchini na duniani kote ambayo ni muhimu kwa maisha na shughuli za wananchi, na pia juu ya masuala muhimu kwa jamii.


Sikiliza Video hii ili nawe ujijengee uelewa
IMG-20240520-WA0021.jpg
IMG-20240520-WA0022.jpg
IMG-20240520-WA0020.jpg
IMG-20240520-WA0019.jpg
IMG-20240520-WA0023.jpg
 
Back
Top Bottom