Mkuu wangu kwa mwenye akili yeyote hawezi kuunga mkono sera zozote zinazoendelea ujenzi wa jengo ambalo tayari halifai kuishi watu.Wakati CCM inasisitiza kujenga juu ya jengo ambalo tayari nguzo zake zimeweka Ufa, Chadema wanakuja na sera mpya za kubomoa nguzo za ujenzi uliopo .. Wanachokifanya CCM ni kuhadaa watu kwamba hali yetu sio mbaya hivyo, uchumi wetu sii mbaya hivyo na kwa bahati mbaya Watanzania hatuna kipimo chochote isipokuwa kulinganisha na umaskini wa maskini wengine.
Mkuu wangu, Tanzania ni sawa na meli inayozama, hakuna sera bora zaidi ya kuokoa kwanza Taifa letu na hakika ni kurudi nyuma na kutazama tumekosea wap.
i
..... Lakini Chadema wanachotupa ni kuvunja nguzo zote zilizopo kuhusiana na ELIMU, AFYA na KILIMO kwa makusudi ya kupambana na adui zetu hao watatu pasipo kuweka matabaka baina yetu na kikubwa zaidi kuweka mbele ufanisi wa sekta zote zinazohusiana na vita hii.
.