Mwalimugeorge
Member
- Apr 26, 2020
- 33
- 13
Chadema ❎
AICT WAZALENDO ❎
NCCR MAGEUZI ☑️
Habari wana jamvi!
Katazo la Mbowe linaonekana kugonga mwamba na kuleta mpasuko mkubwa ndani ya CHADEMA baada ya baadhi ya wabunge wachadema kukataa kile kilichoitwa ukandamizwaji wa demokrasia ndani ya CHADEMA chini ya Mfalme Mbowe!
Mpasuko ndani ya CHADEMA umeenda mbali zaidi baada ya mke wa afisa habari wa chadema bwana Tumaini Makene kutinga bungeni akidai kuwa hatoweza kuyumbishwa na Chama na yeyote ndani ya chadema kwani yeye ni wananchi kwanza!
Hadi kufikia jumatatu ni wabunge wasio pungua watano ndio watakuwa hawapo bungeni baada ya mgogoro zaidi kurndelea kuitesa CHADEMA ya Mfalme Mbowe.
Wasalaam
Sent from my iPhone using Tapatalk
Hii nchi imejikuta kwa miaka mitano hii ni vurugu tupu. Yani kama kuna mtu alikufa 2014 halafu akafufuka 2020 kisha akahadithiwa yaliyotokea atastaajabu.
Imagine spika wa bunge alivyo amemuita mbunge aliyejiuzulu kwa hiari yake ili arudi bungeni. Mbunge alikabidhi kadi ya chama kilichomdhamini ubunge hadharani akapewa kadi ya chama kingine. Leo huyo mbunge anaitwa kuendelea na ubunge wake kwa kutumia kilekile chama alichokikimbia.
Aidha Rais ametoa ndege kwenda kuchukua dawa ambayo masikini hata haijathibitishwa kuwa ni dawa. Rais wa nchi anayetoa dawa hajui hata dozi iweje kwa matumizi. Mbaya zaidi waziri msomi anainywa hadharani! Kama ni sumu? Hivi mbona kama nchi tumefikia kuchanganyikiwa hivi?
Dah acheni abane tu vyombo vya habari maana hivi tunavyovishuhudia ni vituko vya aina yake. Tuna ombwe kubwa la uongozi!
Kipimo cha kutokuwa na Akili timamu ni kushabikia CCM na CHADEMA.
Sent using Jamii Forums mobile app
AICT WAZALENDO ❎
NCCR MAGEUZI ☑️