chama kipya cha walimu

Msingida

JF-Expert Member
Joined
Dec 1, 2010
Posts
10,239
Reaction score
11,731
Niliwahi kupata ujumbe mfupi wa simu kuniarifu kuwa kuna chama kipya cha maafisa elimu (walimu wenye degree) kama mbadala kwa walimu ambao wamechoshwa na ubabaishaji wa cwt.Je ni taarifa za Ukweli?Tunaomba wafungue Web page na facebook ili waanze kujipatia wanachama,maana kuna maswaib makubwa kwa walimu hapa Singida. kuna saccos ya walimu mamilioni yameliwa na hakuna hatua zilizochukuliwa zaidi ya kulindana,watuhumiwa wanaendelea kupeta,hakuna waliofikishwa mahakamani.Chama kipya kinaweza kutupigania walimu tuondokane na madhila ya ukwasi.Kuna walimu wengine wana madeni makubwa kwenye mishahara yao kutokana na mikopo kwenye taasisi za mikopo yenye riba kubwa hadi walimu wengi kuomba kustaafu kabla ya muda kutokana na madeni makubwa.Utafiti ufanyike waalimu waliostaafu kabla ya miaka 60,wengi wao ni kwasababu ya madeni ya kutisha.
Chama kipya cha walimu kinaweza kuwa mkombozi kwa waalimu kutokana na walimu wengi kuteseka na madeni huku saccos yao ikihujumiwa
 

mkuu uko manispaa au halmashauri!??
 
tafuta group ktk Facebook inaitwa umoja wa maafisa elimu Tanzania (UMET) utakuwa umepata unachotafuta.
 
Nilikuwa Halmashauri,nimehamia Manispaa mdaa!!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…