Chama langu Simba hatari inakuja tuchukue tahadhari

Nilikosea hapo mkuu ila nimesharekebisha. Hoja yangu ilikua Si.ba wasidhani wapo kwenye nafasi nzuri sana maana wao wanahitaji ushindi wa aina yoyote kwani sare ya magoli itamaanisha kuyaaga mashindano
Mkuu, mbona unaruka ruka sana, nani kakuambia Simba haiwezi kushinda??kushinda kwako unaona jambo gumu??Unataka tupite bila kushinda??Washindani wa kweli wanajua ili kupita ama kufuzu Kushinda ni sehemu ya wajibu wako!!Ni wajibu wetu Simba kushinda na tutautekeleza ipasavyo!!
 
Tumshauri kocha asifanye majaribio kwa waxhezaji asiokua na uhakika nao yakatokea kama ya mechi na Sevilla
 
Tumshauri kocha asifanye majaribio kwa waxhezaji asiokua na uhakika nao yakatokea kama ya mechi na Sevilla
Mechi na Sevilla Kocha anakuambia alipanga kuwapa nafasi wachezaji wote waonje ladha ya kucheza na team ya kiwango cha dunia, haikuwa mechi ya kimashindano hivyo sio mfano sahihi.

Haya toa Ushauri unataka kikosi kiweje! Ambacho wewe ndio unaona serious?Tiririka sasa tunasoma tutamshauri
 
Asante mdau mtoa uzi tutafanyia kazi, ila nikupe ushauri wa bure unapoenda vitani waza zaidi kushinda kuliko kufeli. Hofu yako ndiyo inawakuta vyura fans hawaiamini timu yao ndiyo maana hawaendi viwanjani hiyo hofu huwapata hata wachezaji pale wanapokosa support kutoka kwa mashabiki.
Simba hiyo hofu huwa hatuna hata pale tunapoona timu yetu ni dhaifu dhidi ya mpinzani rejea timu yetu ikiwa dhaifu msimu wa juzi tulipigwa 3 bila na yanga lakini kwa kuamini siye ndiyo siye nchi hii tulirudisha bao zote jambo ambalo lingekuwa kwa yanga ndiyo wawe wamepigwa goli hizo wangekata tamaa.
Tusiwe watu wakukata tamaa mapema jiamini na adui yako atakuogopa nadhani kujiamini kwa simba ktk uwanja wa mkapa kuliisaidia sana simba kufika robo ccl kwa kuwadindia vigogo wa afrika hadi zahera akawadanganya ndugu zake kuwa simba anapulizia dawa vyumba kumbe hasijue kuwa ni nguvu ya mashabiki iliwafanya wachezaji wajitoe mhanga wasije wakawaangusha
 
Apange kikosi cha mashindano na si majaribio
 
Kwa jinsi walivyocheza simba kule msumbiji kuna hatari wakatolewa mapema tu kwenye michuano hii.

Wakishikiliwa mpaka penalty watatolewa tu maana wanavyocheza ni kama wanalewa kwanza ndiyo wanaingia uwanjani.
 
Ndio kipi hicho?kitaje mkuu
Kupanga kikosi ni kazi ya kocha, siwezi thubutu kumpangia maana sio taaluma yangu. Hii haina maana akipanga kikosi cha hovyo tukapoteza mechi tuache kumlaumu, tutamlaumu hasa ukizingatia bajeti iliyotumika kukusanya kikosi chenyewe

Kama ilivyokua kwa Stars ,Amunike ndie alikua na mandate ya kupanga timu lakini timu ilipoboronga tulijiuliza kwa jinsi alivokua anapanga timu alikua analazimishwa au anapanga mwenyewe!!!! Simba hatutaki litutokee
 
Hii simba ya sasa siyo lethal kama ya msimu uliopita.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…