Chama na kipa Ally ndio walioiondosha Simba mashindanoni

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
13,778
Reaction score
14,214
Wydad imeshuka kiwango, hasa baada ya kuondokewa na wachezaji wake muhimu wa msimu uliopita. Simba wangeweza kufika nusu final kwa kupitia Wydad msimu huu kama sio ujinga wa bench la ufundi, uongozi wa Simba, Chama na Ally Salim.

Wydad waliokolewa na golikipa wao kudaka mikwaju 2 iliyopigwa vizuri na kapo Kapombe na Chama kitu ambacho Ally Salim hakuweza kukifanya kutokana na uchanga wake golini.

Uongozi wa Simba na bench la ufundi kuacha kumtumia Beno Kakolanya kwasababu za kijinga, kipuuzi, kibwege, unsporting na kichawi kukaa langoni kudaka penati na kumuamini kijana kinda kulisababisha Simba kuingia hasara kubwa sana ya kutolewa mashindanoni na timu dhaifu ya Wydad, Ningekuwa mimi ni mo ningemsaka aliyesema Beno kipa namba 2 asikae golini kwenye mashindano haya makubwa baada ya Manula kuumia.

Chama na Kapombe hawakuwa makini na kazi Yao pia ingawa penati huwa hazina mwenyewe lakini "why us" every day tutolewe robo final?

Bench la ufundi lilipaswa kumwingiza Beno kudaka japo penati TU badala ya mtoto Ally ambae aliteseka sana kujirusha chini kwa namna ileile kwa penalti zote.

Swali ni je, Simba itakuwa na ubavu wa kumzuia Inonga abaki Simba? Inonga pekee ndiye aliyepunguza idadi ya magoli siku Ile.
 
Ngoja waje hapa mapovu kibao wana hasira sana
 
Ila binadamu bwana, kweli tenda wema amsha zako! Huyu huyu Chama kawabeba mabegani mara ngapi leo mnamnanga kwa kukosa penalt? Penalt haina mwenyewe kaka... Anyway.. huo ni ugomvi wenu madunduka!!
 
Kwa upande wangu naona hata kocha pia kachangia.
Ndani ya mchezo wa dakika 90, kocha angekuwa na mkakati wa kutafuta goli angefanikiwa kulipata, kuna muda waarabu walikuwa wameshachanganyikiwa na kukata tamaa na kupoteza umakini kiasi kwamba hata pass zao zinatoka nje kirahisi tu. Hapo angewaingiza watu wenye spidi kama Sakho na phiri kuongeza nguvu, na pia kwavile wanaamua kujilipua lazima Onyango umtoe umuingize hata Kenedy ili ikitokea mashambulizi ya kustukiza kusiwe na shida.

Baada ya dakika 90 kutaka kuisha, kocha angemuingiza Beno kakolanya ili akadake kwenye hatua ya penati. Beno angeweza kusaidia hata ku save penati ili kurudisha wachezaji mchezoni.

Maoni yangu....
 
Acha bangi zako utopolo.
Sisi wana Simba hatuna cha kuwadai wachezaji wetu wala benchi la ufundi.

Sent from my Infinix X626 using JamiiForums mobile app
 
Umeongea point sana. Wydad kwa sasa wameshuka sana kiwango,baada ya kuondokewa wachezaji wake na kocha.

Simba wangeingia kwa miguu yote bila kuingia kwa hofu ksbb tu ya jina la Wydad bingwa mtetezi. Simba ilikuwa wapite nao tu hawa,ilikuwa size kabisa. Simba wakaogopa ile history ya Wydad kwao na wale mashabiki wake.

Ona Simba walivyoamua kushambulia kwa muda lango la Wydad,mashabiki wake walinywea,maana yake tayari nao waliingiwa na ubaridi. Kabisa hii nafasi Simba ilikuwa yao. Hata Wydad wenyewe hawaajaamini ksbb nao wamejitambua udhaifu wao.

Beno ilikuwa kabisa akae langoni,eti Beno atatufungisha. Ujinga kabisa na uchawi tu,sasa kwa nini walisafiri nae?. Wanakaa nae wa nini kama hawamtaki?.
 
UTAONGEA YOTE mkuu lakini mchawi ni.........



KUHUSU SUALA LA USAJILI.

NASHAURI YAFUATAYO.

1. NIMESIKITIKA UONGOZI KUMUACHA BENO KAKOLANYA.
Kupata Golikipa aina ya kakolanya itakuwa mtihani mkubwa sana.
Sijui kama Tutakuwa na Golikipa No 2 mwenye ubora wa Kakolanya.
Sijui kama hatutaenda Nje kutafuta mbadala wa MANURA.

2.UBAHILI NA 10% KWENYE IDARA YA USAJILI.
tumeshuhudia wakiletwa wachezaji cheep mno kwenye usajili wachezaji wenye uwezo mdogo sana na gharama ndogo sama

3. USAJILI WA QUALITY NDOGO NA KUKOSA SCAUT WAZURI.

I. Ismail sawadogo.
II .mohamed Qottara
III. Augustino Okkrah. (9)
IV. Peter Banda.
V. Sadio Kanute atafutiwe mbadala(8)
VI. Sackho nae Atupishe.

4. WACHEZAJI WAZAWA NAPO NI SHIDA.
Changamoto ya umli.
Nyoni, Boko, mkude,
Viwango vidogo.
Kapama, Gadiel, Mwanuke,

MASHABIKI TUMECHOSHWA KUISHIA ROBO FAINALI.
TUNA HELA ZA KUTOSHA KWA AJILI YA USAJILI.
HELA YA SUPER CUP 4 BILION.
HELA YA CAF. CAFCL 2 BILION

UONGOZI PUNGUZENI UBAHILI
ROBERTINO ASAJILI.
 
Ukiona mtu anaanzisha nyuzi za kuwaponda wachezaji huyo mpuuzieni sio mwenzetu...hajui mpira kuwa
siku zote sio alhamis..
Au ni utoooo
 
Wydad ata mkirudiana wiki ijayo tena Kwa mechi mbili bado watawatoa, nusu fainali haziendi timu za mchongo Kwa kutegemea Ulozi.
Tulia na kombe la lako la kushirikishwa..manajitapa na kuwafunga mito ilojichokea..
 
Acha bangi zako utopolo.
Sisi wana Simba hatuna cha kuwadai wachezaji wetu wala benchi la ufundi.

Sent from my Infinix X626 using JamiiForums mobile app
Sio kweli kaka, tunawadai nusu fainali. Haiwezekani robo finali 4 zisizae nusu final moja. Lugha hiyo ni lugha ya kujikaza sana na maumivu. Kuna mpiuzi mmoja anadai kuwa eti tumekufa kiume, amesahau kuwa hii ni robo fainali ya 4, amesahau kuwa timu imepoteza 10ml za mama na mabilioni ya CAF kizembe. Beno hapangwi kudaka eti kwasababu anatakiwa na singida United, huko Ulaya na kwingineko wachezaji wanawaniwa na timu nyingine lakini wanaendelea kukiwasha kwenye timu zao. Kivuli Cha Yanga kinatutesa sana.
 
Ukiwachana ukweli wanakasrika , lakni ukweli ndo huo kama Simba imeshindwa kuingia semi final dhidi ya timu dhaifu ya wydad sjui kama watapata hii ngekewa tena , inashangaza mashabiki wa Simba walikuwa na hofu kuwa wydad ni timu kubwa na hii inferiority complex ilikuwa mpak Kwa bench la ufundi kushindwa kusaka goli ugenini na kujisifia kuzuia ...

Alaf mtu anakuja et timu ipelekwe bungeni , kila mwaka unaishia robo final unajisifu
 
Juzi tu mlikuwa mkikesha kutoa list ya matokeo ya Wydad jinsi anavyotoa vipigo akiwa kwake, leo mmegeuka mnasema imeshuka kiwango πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚





Ma-loosers mna taabu kwel kwel 🀣🀣🀣🀣
 
Hiyo widad unayo ita dhaifu si ndo iliwafunga vibonde mnacheza nao kwenye kombe lenu la michongo magoli sita bila ?
 
Tulia wewe usije kujiua Bure,that's why inaitwa sports,it's win or loose,acha kitoa povu.Mboma Arsenal.hawana.mapovu na ubingwa Karibu wanaupoteza dakika za.mwisho na city anaelekea kuchukua triple.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…