Chama tawala dhidi ya akili za wapinzani

Chama tawala dhidi ya akili za wapinzani

Nzi ni nyuki mjinga

JF-Expert Member
Joined
Jan 13, 2020
Posts
1,073
Reaction score
1,556
Nimekuwa nikipitia na kuchunguza siasa za nchi yetu na nasikitika kusema kuwa hapa JF, home of great thinkers kuna wakosoaji na wapinzani mahiri sana wa utawala wa chama tawala lakini ni wakosoaji wasiobadilika, wamekuwa kama watoto wa kambo na msemo wa baba/mama angekuwepo tusingekuwa na maisha haya, mara nyingi huu msemo hutamkwa bila kujali ukubwa au udogo wa mateso wanayopitia, huenda hata mzazi/wazazi wangekuwepo mateso yangekuwa vile vile au zaidi.

Natamani ningewataja hawa wapinzani wakosoaji au niwaite watoto wa kambo lakini sababu wanafahamika ngoja niwaache.

Hoja yangu hapa ni hii, kwanini unakosoa kwa mtindo ule ule ila hauna matokeo na ww mkosoaji hubadiliki. Kila awamu unaponda na kuponda na kuponda unaishia kuota sugu tu bila matokeo.

Chama tawala kina malengo makuu yafuatayo:
1. Kutawala na kuendelea kutawala bila kujali wewe mkosoaji unalia lia kwa mtindo upi.
2. Kuhakikisha upinzani ni dhaifu na dhaifu sana
3. Kuhakikisha wananchi wanazungumza kuhusu chama tawala iwe ni kwa kiki, matukio, maigizo au vyovyote lakini wakizungumze.

Sasa changamoto moja tu ya chama tawala ni kuhusu nani apewe usukani wa kuhakikisha hayo niliyoyataja yanatimia, na hapa ndipo wakosoaji na wapinzani wanapofeli, chama tawala kimekuwa kikitumia hii changamoto kama mtaji wa kisiasa na wakosoaji pamoja na upinzani huwa wanaingia wazima wazima kushindanisha chama tawala vs chama tawala.

Hapa wamekuwa wakiendelea kukisaidia chama tawala kuendelea kufikia malengo ya kutawala kiurahisi wakidhani wanawatesa watawala. Hizi ndo akili za nzi kudhani atatengeneza asali kwa kushinda jalalani na chooni.

Uchaguzi unakuja, inasemekana chama tawala kimepasuka na wakosoaji wanaamini hivyo, kuna vita kubwa sana ya chama tawala dhidi ya chama tawala inakuja na mshindi anaweza kuwa chama tawala halafu wale wakosoaji baada ya kuchagua upande mmojawapo wa chama tawala na kuwasaidia kuendelea kutawala watarudi humu na wataendelea kupayuka huku JF juu ya demokrasia, umaskini, ukandamizaji, uonevu ufisadi n. K.

Niwatakie kila la heri kwenye mchezo mtakaoucheza 2020.
 
Back
Top Bottom